Tahasusi Za Michezo Kidato Cha Tano (Combination za Michezo Kidato cha Tano)
Katika mfumo wa elimu ya sekondari nchini Tanzania, kuchagua tahasusi ya kidato cha tano ni hatua muhimu inayochangia sana mustakabali wa taaluma za wanafunzi. Wanafunzi wa kidato cha tano wanapewa fursa ya kuchagua mchepuo maalum unaolingana na ndoto na malengo yao ya baadaye. Moja ya michepuo iliyopo kwa sasa ni Tahasusi za Michezo, ambazo zinawapa wanafunzi nafasi ya kuchanganya masomo ya kitaaluma na vipaji vyao vya michezo.
Uamuzi wa kuchagua tahasusi sahihi sio tu unachangia mafanikio ya mwanafunzi katika kidato cha tano na sita, bali pia unaathiri moja kwa moja fursa za kujiunga na vyuo vikuu au kupata mafunzo ya kitaaluma. Tahasusi za michezo zinalenga kuendeleza ujuzi wa mwanafunzi katika masomo yanayohusiana na michezo huku pia wakipata maarifa mengine ya msingi kama vile lishe, muziki, na lugha.
Kwa wale wanaopenda kuendeleza vipaji vyao vya michezo huku wakiwa na malengo ya kusomea masomo mengine yanayohusiana, tahasusi hizi ni chaguo bora. Inawapa wanafunzi fursa ya kujiandaa vyema kwa taaluma kama vile elimu ya michezo, afya, lishe, muziki, au hata kozi zinazohusiana na ualimu wa michezo.
Orodha ya Tahasusi za Michezo Kidato cha Tano
- Biology, Food and Human Nutrition and Sports (BNS)
- English Language, Music and Sports (LMS)
- Kiswahili, Music and Sports (KMS)
- Fasihi ya Kiswahili, Music and Sports (FaMS)
- Literature in English, Music and Sports (LiMS)
- French, Music and Sports (FMS)
- Arabic, Music and Sports (ArMS)
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka maoni yako