Ligi Kuu NBC 2025/2026 Kuanza Septemba 16: Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza rasmi kuwa msimu mpya wa 2025/2026 wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara utaanza Septemba 16, 2025.
Ligi Kuu NBC 2025/2026 Kuanza Septemba 16
Tangazo hili linawapa muda wadau wote wa soka nchini kujipanga ipasavyo, ikiwa ni pamoja na klabu zinazoshiriki, mashabiki, waamuzi na wadhamini. Kwa mujibu wa TFF, maandalizi ya ratiba ya mechi na usajili wa wachezaji yanaendelea kwa mujibu wa kanuni za ligi/Ligi Kuu NBC 2025/2026 Kuanza Septemba 16.
Msimu wa 2025/2026 wa ligi hiyo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na maandalizi madhubuti yanayofanywa na vilabu vikubwa vya Young Africans SC, Simba SC, Azam FC na nyinginezo zinazoimarisha uwepo wao kwa kusajili wachezaji wa kitaifa na kimataifa.

Aidha TFF imesisitiza kuwa vilabu vyote vinapaswa kukamilisha taratibu za usajili kabla ya tarehe rasmi ya kufungwa kwa muda wa usajili pamoja na kuhakikisha viwanja vyao vinakidhi viwango vya kimataifa vya kuandaa mechi za ligi hiyo.
Weka maoni yako