Azam FC Kukamilisha Usajili wa Sadio Kanouté

Azam FC Kukamilisha Usajili wa Sadio Kanouté: Klabu ya Azam FC ya Tanzania iko katika hatua za mwisho za kumsajili kiungo mshambuliaji wa Mali Sadio Kanouté (28) ambaye kwa sasa yuko huru. Kanouté anatarajiwa kujiunga rasmi na Azam FC baada ya kuachana na klabu ya JS Kabylie ya Algeria.

Azam FC Kukamilisha Usajili wa Sadio Kanouté

Kanouté aliyeichezea Simba SC katika misimu iliyopita ya Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa, anarejea katika soka la Tanzania, safari hii akiwa chini ya usimamizi wa Azam FC.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, uongozi wa Azam FC unaamini uzoefu wa Kanouté katika michuano ya kimataifa, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika, utakuwa na manufaa makubwa kwa klabu hiyo inayopania kuimarika katika msimu ujao wa 2025/2026.

Azam FC Kukamilisha Usajili wa Sadio Kanouté
Azam FC Kukamilisha Usajili wa Sadio Kanouté

Kanouté aliichezea Simba SC kwa mafanikio kabla ya kujiunga na JS Kabylie. Wakati akiwa Simba, alijidhihirisha kwa uwezo wake mkubwa wa kuongoza mashambulizi kuanzia katikati ya uwanja, kufanya mashambulizi yenye ufanisi na kuisapoti timu katika mechi muhimu za mashindano ya ndani na kimataifa.

CHECK ALSO:

  1. KIKOSI Cha Taifa Stars Leo vs Burkina Faso 02/08/2025
  2. Matokeo ya Taifa Stars vs Burkina Faso Leo 02/08/2025
  3. Ligi Kuu NBC 2025/2026 Kuanza Septemba 16
  4. Yanga SC Kukamilisha Uhamisho wa Clement Mzize kwa Dola 900,000