Kapombe Mchezaji Wenye Umri Mkubwa Zaidi Taifa Stars Kwenye CHAN 2024/25: Katika Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024, timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ina mchanganyiko wa wachezaji wazoefu na chipukizi, inayoakisi uwiano kati ya uzoefu na vipaji vinavyochipukia.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Shomari Salum Kapombe na Hussein Salum Masalanga ndio wachezaji wakongwe kwenye timu hiyo kila mmoja akiwa na umri wa miaka 33.
Kapombe Mchezaji Wenye Umri Mkubwa Zaidi Taifa Stars Kwenye CHAN 2024/25
-
Kapombe alizaliwa Januari 28, 1992.
-
Masalanga alizaliwa Machi 4, 1992.
Kwa upande mwingine, wachezaji wenye umri mdogo zaidi ni Jammy Jammy na Wilson Nangu, ambao wote wamezaliwa mwaka 2006:

-
Jammy Jammy: Julai 15, 2006
-
Wilson Nangu: Julai 25, 2006
Mchanganyiko huu wa umri ni faida kubwa kwa timu. Wachezaji wenye uzoefu kama Kapombe na Masalanga wanatoa uongozi na mwelekeo uwanjani, huku wachezaji wachanga kama Jammy na Nangu wakileta kasi, nguvu, na ari mpya ya ushindani.
Kwa CHAN 2024, kocha na wafanyikazi watategemea mchanganyiko huu kupata usawa wa matokeo mazuri, huku wachezaji wachanga watapata fursa ya kujifunza kutoka kwa wakongwe wa timu.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako