CAF Champions League 2025/26 Simba, Yanga na Mlandege FC: Droo ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) 2025/26 imekamilika, na wawakilishi wa Tanzania Bara na Zanzibar sasa wanawafahamu wapinzani wao katika harakati za kuwania ubingwa wa Afrika.
CAF Champions League 2025/26 Simba, Yanga na Mlandege FC
Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Young Africans SC (Yanga SC) watamenyana na wababe wa Angola, Wiliete Benguela SC katika pambano linalotarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na historia na ubora wa wapinzani wao.
Wapinzani wa jadi wa Yanga, Simba SC watamenyana na Gaborone United ya Botswana, timu yenye uzoefu wa michuano ya kimataifa ambayo imekuwa ikikutana mara kwa mara na wapinzani wa Afrika Kusini.

Kwa upande wa Zanzibar, mwakilishi wao, Mlandege FC, itamenyana na Ethiopia Insurance ya Ethiopia, pambano litakalowapa fursa taifa hilo la visiwani humo kuonesha vipaji vyao katika medani ya kimataifa. Kwa mujibu wa kalenda ya CAF, mechi za mkondo wa kwanza wa hatua ya awali zinatarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 19 na 21, 2025, na mechi za mkondo wa pili kati ya Septemba 26 na 28, 2025.
Mechi za Hatua ya Awali CAFCL 2025/26 kwa Wawakilishi wa Tanzania na Zanzibar:
-
🇪🇹 Ethiopia Insurance 🆚 Mlandege FC (Zanzibar)
-
🇧🇼 Gaborone United 🆚 Simba SC (Tanzania)
-
🇦🇴 Wiliete Benguela 🆚 Yanga SC (Tanzania)
CHECK ALSO:








Weka maoni yako