UEFA Super Cup 2025, PSG vs Tottenham Hotspur Leo Agosti 13: Jumatano, Agosti 13, 2025, pazia litafunguliwa rasmi kuhusu UEFA Super Cup, ambayo itawaleta pamoja mabingwa wa mashindano makubwa ya vilabu barani Ulaya.
UEFA Super Cup 2025, PSG vs Tottenham Hotspur Leo Agosti 13
Paris Saint-Germain (PSG), mabingwa wa UEFA Champions League 2024/25, watamenyana na Tottenham Hotspur, mabingwa wa UEFA Europa League msimu wa 2024/25, katika mechi inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na burudani.
Mechi itaanza saa 4:00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki na itafanyika kwenye Uwanja wa Bluenergy (Stadio Friuli) huko Udine, Italia. Uwanja huu ni nyumbani kwa Udinese, klabu katika Serie A ya Italia.
UEFA Super Cup ni kombe la kifahari linalowaleta pamoja mabingwa wa mashindano mawili makubwa ya Ulaya. Kwa PSG, hii ni nafasi ya kuendeleza ubabe wao wa Ulaya baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku kwa Tottenham, ni nafasi ya kuthibitisha kwamba mafanikio yao ya Ligi ya Europa hayakuwa bahati tu.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako