Simba Kuwaaga Wachezaji wa Zamani Bocco na Mkude | Ofisa habari wa Simba SC, Ahmed Ally, alitangaza kuwa siku ya Simba Day mwaka huu itakuwa maalum kwa mashabiki na familia ya Wekundu hao wa Msimbazi. Tukio hilo litakalofanyika Septemba 10, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, si tu litakuwa na burudani na uzinduzi wa kikosi kipya, bali pia kuwaenzi wachezaji wa zamani waliochangia kwa kiasi kikubwa klabu hiyo.
Simba Kuwaaga Wachezaji wa Zamani Bocco na Mkude
Kwa mujibu wa Semaji Ahmed Ally, mwaka huu Simba SC itakabidhi tuzo maalum za heshima kwa nyota waliong’ara ndani ya klabu hiyo akiwemo John Bocco, mshambuliaji nyota wa klabu hiyo na nahodha wa muda mrefu.
Aidha, tukio kubwa litakalowasukuma mashabiki ni kumuaga rasmi kiungo mkongwe aliyeichezea Simba SC kwa miaka 15 mfululizo, Jonas Gerald Mkude. Mkude amekuwa tegemeo kwa muda mrefu katika safu ya kiungo, akiwa ameshinda vikombe kadhaa vya ligi na kushiriki katika kampeni za kimataifa za CAF.

Ahmed Ally alibainisha kuwa klabu itaendelea na utaratibu wa kuwaaga kwa heshima wachezaji wake wa muda mrefu, akisisitiza kuwa “malenge wetu wataendelea kuagwa taratibu pale tutakapopata nafasi.” Pia alitania kuwa mchezaji ambaye mashabiki wanamsubiri kuagwa rasmi, ataagwa “mara baada ya kumaliza kuchukua pensheni yake.”
Simba Day 2025 inatarajiwa kuwa zaidi ya tamasha tu. Ni siku ya kumbukumbu, heshima na historia ambapo mashabiki watashuhudia kuwaenzi wachezaji walioitumikia klabu hiyo kwa uaminifu na mafanikio makubwa. Hii ni fursa ya kipekee kwa mashabiki kusherehekea historia na kutayarisha mustakabali mpya wa Simba SC.
SOMA PIA:
Weka maoni yako