Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2024/25 Online

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2024/25 Online

Mwaka hadi mwaka, maelfu ya wanafunzi nchini Tanzania huhitimisha safari yao ya elimu ya msingi kwa kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) almaharufu kama mtihani wa darasa la saba.

Mtihani huu, unaosimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), ni kipimo muhimu cha uelewa wa wanafunzi katika masomo mbalimbali na huamua hatua inayofuata katika maisha yao ya kitaaluma. Huu ni wakati uliojaa hofu na matarajio makubwa kwa wanafunzi, wazazi, na walezi wanaosubiri kwa hamu kuona matunda ya juhudi zao.

Kutokana na mabadiliko makubwa ya tehema, NECTA imerahisisha zaidi upatikanaji wa matokeo ya darasa la saba kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Sasa, badala ya wanafunzi na wazazi/walezi kulazimika kusubiri matangazo rasmi ya matokeo kwenye machapisho ya magazeti au foleni ndefu mashuleni, sasa wanaweza kuangalia matokeo ya PSLE 2024/25 kwa haraka na kwa ufanisi zaidi mtandaoni. Hapa tumekuletea maelekezo rahisi ya jinsi ya kuangalia matokeo ya darasa la saba online ili kukusaidia kujua hatua muhimu za kupata matokeo mtandaoni.

Hatua za Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba Online:

Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA

Fungua kivinjari chako cha wavuti (kama vile Chrome, Firefox, au Safari) na uandike anwani ifuatayo kwenye upau wa anwani: https://necta.go.tz/ Hii itakuelekeza kwenye tovuti rasmi ya Baraza la Mitihani la Tanzania.

Nenda kwenye Sehemu ya “Results”

Kwenye ukurasa wa mwanzo wa NECTA, utaona menyu kuu iliyo na viungo mbalimbali. Tafuta na ubofye kiungo cha “Matokeo”. Menyu kunjuzi itaonekana ikiwa na orodha ya mitihani mbalimbali.

Chagua “Matokeo ya PSLE”:

Katika orodha ya mitihani, chagua “Matokeo ya PSLE” au “Matokeo ya Darasa la Saba”. Hii itakuelekeza kwenye ukurasa maalum wa matokeo ya darasa la saba.

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba

Chagua Mwaka wa Mtihani

Ukurasa wa matokeo ya PSLE utakuonyesha chaguo la kuchagua mwaka wa mtihani. Hakikisha unachagua mwaka sahihi, ambao ni “2024/25” kwa matokeo ya mwaka huu.

Kuangalia matokeo ya mtihani wa kumaliza shule ya msingi

Chagua Mkoa na Wilaya

Ili kurahisisha utafutaji, NECTA hupanga matokeo kwa mkoa na wilaya. Chagua mkoa na kisha wilaya ambapo mwanafunzi alifanya mtihani.

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Shule ya Msingi

Tafuta Jina la Shule

Orodha ya shule zote zilizopo katika wilaya uliyochagua itaonekana. Pitia orodha hiyo kwa makini ili kupata jina la shule ya mwanafunzi. Ili kurahisisha utafutaji, unaweza kutumia kipengele cha kutafuta (search) kwenye kivinjari chako. Kwa kawaida, unaweza kufanya hivyo kwa kubonyeza Ctrl + F (kwenye Windows) au Command + F (kwenye Mac) na kuandika jina la shule.

Tazama Matokeo

Mara tu unapopata jina la shule, bofya juu yake. Hii itafungua ukurasa mpya ulio na orodha ya wanafunzi wote wa shule hiyo na matokeo yao. Tafuta jina la mwanafunzi ili kuona matokeo yake.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Malengo Ya Mitihani Ya Necta Kidato Cha Nne (CSEE) Na Kidato Cha Sita (ACSEE)
  2. Mambo Anayoweza kufanya Muhitimu wa Darasa la Saba Akisubiri Matokeo
  3. Tahasusi Za Lugha Kidato Cha Tano
  4. Sifa Za Kujiunga Na Degree Kutoka Diploma 2024/2025
  5. Orodha ya Shule za Sekondari za Jeshi Tanzania
  6. Michepuo ya Sayansi Kidato cha Tano