Nafasi 5 Za Kazi Msaidizi Wa Kumbukumbu Halmashauri Ya Wilaya Ya Kyela

Nafasi 5 Za Kazi Msaidizi Wa Kumbukumbu Halmashauri Ya Wilaya Ya Kyela

Halmashauri ya Wilaya ya Kyela imetangaza nafasi tano (5) za kazi kwa nafasi ya Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II. Nafasi hizi zimetangazwa baada ya Halmashauri hiyo kupata kibali cha ajira mbadala kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Nafasi hizi ni kwa Watanzania wenye sifa stahiki na wanaotaka kujiunga na huduma za umma.

Watanzania wenye sifa zinazotakiwa wanahimizwa kutuma maombi yao haraka iwezekanavyo. Halmashauri ya Wilaya ya Kyela inatoa fursa hii kwa wale wenye nia ya kujiunga na huduma ya umma, hasa kwa kazi inayohusiana na utunzaji wa kumbukumbu katika taasisi za serikali.

Majukumu ya Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II

Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II atahusika na majukumu mbalimbali yanayohusiana na utunzaji wa kumbukumbu, ni pamoja na:

  • Kuorodhesha barua zinazoingia kwenye masjala kupitia regista maalum (Incoming Correspondence Register).
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi katika regista ya barua zinazotoka (Outgoing Correspondence Register).
  • Kusambaza na kupokea majalada kutoka kwa Watendaji wa taasisi husika (Action Officers).
  • Kurudisha majalada kwenye shabaka au kabati la majalada yanapohifadhiwa.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi (File tracking) kuhakikisha ufanisi wa upatikanaji wa kumbukumbu.

Sifa za Mwombaji

Waombaji wanapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

  • Elimu: Mwombaji awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) na awe na Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
  • Ujuzi wa Kompyuta: Mwombaji anatakiwa awe na ujuzi wa kompyuta, hasa katika programu zinazohusiana na utunzaji wa kumbukumbu.
  • Umri: Mwombaji awe na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45.

Masharti ya Jumla ya Ajira

Masharti haya ni muhimu kwa waombaji wote:

  • Mwombaji awe raia wa Tanzania.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na wanapaswa kueleza aina ya ulemavu wao kwenye fomu ya maombi.
  • Curriculum Vitae (CV): Waombaji wote wanatakiwa kuambatanisha CV yenye taarifa za kina, anwani za barua pepe, namba ya simu, pamoja na majina ya wadhamini watatu.
  • Cheti cha kuzaliwa: Waombaji wote wanapaswa kuambatanisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria au Wakili.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa umma wanapaswa kupitisha maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.

Vigezo Muhimu vya Kuambatanisha na Maombi

Waombaji wote wanatakiwa kuzingatia:

  • Cheti cha Kidato cha Nne na/au Kidato cha Sita.
  • Vyeti vya kitaaluma (Stashahada ya Utunzaji Kumbukumbu).
  • Vyeti vilivyothibitishwa kwa wale waliosoma nje ya nchi, ambapo ni lazima vyeti vyao viwe vimeidhinishwa na mamlaka husika kama TCU, NACTE, au NECTA.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Maombi ya nafasi hizi yanapaswa kutumwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa ajira unaopatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kupitia https://portal.ajira.go.tz. Mwombaji anatakiwa kuhakikisha anatumia mfumo huu rasmi wa ajira na kuzingatia tarehe ya mwisho ya kutuma maombi, ambayo ni 03 Novemba, 2024.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwa anuani ya:

MKURUGENZI MTENDAJI (W)
Halmashauri ya Wilaya ya KYELA
S.L.P 320, Kyela
Mbeya, Tanzania.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Nafasi 10 Za Kazi Msaidizi Maendeleo Ya Jamii Halmashauri Ya Wilaya Ya Kyela
  2. Nafasi Mpya za Kazi Mbalimbali TANROADS Njombe, Mwisho 21 oktoba 2024
  3. Nafasi Mpya za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa September 2024
  4. Nafasi Mpya za Kazi Mbalimbali TANROADS Njombe, Mwisho 21 oktoba 2024
  5. Nafasi Mpya za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa September 2024