Simbu Ashinda Medali ya Dhahabu Ubingwa wa Dunia wa Marathon Tokyo 2025

Alphonce Simbu Ashinda Medali ya Dhahabu Ubingwa wa Dunia wa Marathon Tokyo 2025, Aipa Tanzania Heshima.

Mwanariadha wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu aliweka historia ya kutwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya Riadha ya Dunia yaliyofanyika Tokyo, Japan. Ushindi huu mkubwa umeipa Tanzania heshima ya kipekee katika anga ya kimataifa ya riadha.

Simbu Ashinda Medali ya Dhahabu Ubingwa wa Dunia wa Marathon Tokyo 2025

Katika shindano hilo, Simbu aliongoza mbio za marathon za kilomita 42, akionyesha uvumilivu na ufundi mkubwa. Ushindi wake unachukuliwa kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha hadhi ya Tanzania katika riadha hasa mbio za masafa marefu ambazo zimetawaliwa na mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Simbu Ashinda Medali ya Dhahabu Ubingwa wa Dunia wa Marathon Tokyo 2025
Simbu Ashinda Medali ya Dhahabu Ubingwa wa Dunia wa Marathon Tokyo 2025

Mara baada ya ushindi huo mkimbiaji mwenzake Choughule alimpongeza Simbu kwa mafanikio yake makubwa. Alisema:

“Hongera Ndugu yetu Alphonce Simbu kwa kushinda Ubingwa wa Dunia Marathon Kilometa 42 zilizofanyika Tokyo, Japan. Ushindi huu ni fahari ya taifa letu na mfano bora kwa wanariadha chipukizi.”

Simbu, ambaye ameendelea kuwa kinara wa Tanzania katika mbio za kimataifa, sasa anatajwa kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wanaotamani kuingia kwenye riadha. Ushindi huu unatarajiwa pia kuamsha ari mpya kwa wadau wa michezo nchini kuongeza uwekezaji katika riadha na kusaidia vipaji vipya.

CHECK ALSO:

  1. FIFA Yaondoa Adhabu ya Usajili Fountain Gate
  2. Oscar Mirambo Ateuliwa Kukaimu Nafasi ya Wilfred Kidao
  3. Simba vs Fountain Gate Leo Viingilio vya Mchezo Septemba 25, 2025
  4. Matokeo ya Azam FC vs Mbeya City Leo 24/09/2025