Ratiba ya CRDB Bank Federation Cup 2025/2026: Michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (FA) ambayo pia inajulikana kama Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB, ni mashindano makubwa ya mtoano katika soka la Tanzania. Vilabu vya ligi mbalimbali vinashiriki ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza, Daraja la Pili na timu za Visiwani Zanzibar.
Kusudi kuu la mashindano ni kuamua bingwa wa kitaifa kupitia mfumo wa mtoano, na timu itafuzu moja kwa moja kwa raundi inayofuata baada ya ushindi. Mashindano hayo pia yanatoa fursa kwa klabu inayoshinda kushiriki Kombe la Shirikisho la CAF, na kuongeza heshima na umuhimu wake katika mazingira ya soka ya Afrika/Ratiba ya CRDB Bank Federation Cup 2025/2026.
Ratiba ya CRDB Bank Federation Cup 2025/2026
Bado ratiba rasmi ya mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB kwa msimu mpya wa 2025/26 hayajatolewa. Kwa mujibu wa kalenda ya TFF inaonyesha mashindano ya CRDB Federation Cup yataaza rasmi desemba 5, 2025 na fainali kuchezwa 27 mei 2026
Hatua ya 64 Bora
6-7 December 2025
Hatua ya 32 Bora
13-15 March 2026
Hatua ya 16 Bora
28-30 April 2026
Robo fainali
9-11 May 2026
Nusu fainali
16-17 May 2026

Fainali
27 May 2026
Washindi wa Kombe La Shirikisho Tanzania la CRDB kwa miaka ya hivi karibuni
2020–21: Simba SC
2021–22: Young Africans FC (Dar es Salaam) 3-3 (aet, 4–1 pens) Coastal Union F.C. (Tanga)
2022–23: Young Africans FC (Dar es Salaam) 1-0 Azam F.C. (Dar es Salaam)
2023–24: Young Africans FC (Dar es Salaam) 0-0 (aet, 6–5 pens) Azam F.C. (Dar es Salaam)
2024–25: Young Africans (Dar es Salaam) 2–0 Singida Black stars (Singida)
CHECK ALSO:
Weka maoni yako