Simba SC Vs Gaborone Leo 28/09/2025 Saa Ngapi?

Simba SC Vs Gaborone Leo 28/09/2025 Saa Ngapi?, Klabu ya Simba SC inashuka dimbani leo jioni kupepetana na Gaborone United ya Botswana katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Wekundu wa Msimbazi wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na faida ya ushindi wa bao 1–0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Gaborone, Botswana, wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally, mchezo wa leo utafanyika bila mashabiki kufuatia adhabu iliyowekwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Klabu hiyo imeandaa kituo maalum cha kuonesha mechi hiyo kwa mashabiki katika eneo la Mwembe Yanga, Temeke, ili kurahisisha wapenzi wa timu hiyo kufuatilia pambano hilo.

Kocha wa muda wa Simba SC, Hemed “Morocco” Suleiman, amesema kikosi chake kipo tayari kwa changamoto hiyo na kwamba kimejipanga kuhakikisha kinatumia vyema faida ya uwanja wa nyumbani ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Aidha, Gaborone United nao wamewasili jijini Dar es Salaam wakiwa na matumaini ya kupindua matokeo, huku wakiahidi kupambana hadi dakika ya mwisho.

Simba SC Vs Gaborone Leo 28/09/2025 Saa Ngapi?

Simba SC Vs Gaborone Leo 28/09/2025 Saa Ngapi?
Simba SC Vs Gaborone Leo 28/09/2025 Saa Ngapi?

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, na mshindi wa jumla atafuzu hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2025/26.

CHECK ALSO:

  1. Ratiba ya CAF Klabu Bingwa Afrika 2025/2026
  2. Ratiba ya Simba SC Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2025/2026
  3. Ratiba ya Yanga SC 2025/2026
  4. Kikosi cha Singida Black Stars Leo vs Rayon Sports 27/09/2025