Serikali Yatangaza Nafasi 41,500 za Ajira Mpya kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza rasmi nafasi 41,500 za ajira mpya katika sekta mbalimbali za umma, ikiwa ni sehemu ya juhudi endelevu za kukabiliana na upungufu wa watumishi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Serikali Yatangaza Nafasi 41,500 za Ajira Mpya kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026
Tangazo hilo limetolewa leo, tarehe 10 Oktoba 2025, jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi. Amesema ajira hizo zitatolewa kwa awamu mbili, katika mwaka wa fedha 2024/2025 na 2025/2026, huku mchakato mzima wa ajira ukitarajiwa kukamilika ifikapo Novemba 2025.
Bw. Mkomi alieleza kuwa mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, yenye lengo la kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi hasa katika sekta muhimu za kijamii na kiuchumi.
Mgawanyo wa Nafasi za Ajira Mpya
Katibu Mkuu Mkomi alibainisha idadi ya nafasi zitakazotolewa kwa kada mbalimbali kama ifuatavyo:
-
Elimu – Nafasi 12,176
-
Afya (ngazi ya serikali za mitaa) – Nafasi 10,280
-
Kilimo – Nafasi 470
-
Mifugo – Nafasi 312
-
Uvuvi – Nafasi 47
-
Vyombo vya Ulinzi (Polisi, Magereza, Zimamoto, na Uhamiaji) – Nafasi 7,000
Amesema ajira hizo zitakuwa na kipaumbele kwa sekta zinazotoa huduma za moja kwa moja kwa wananchi, kama shule, hospitali, na taasisi za usalama, ili kuongeza ufanisi na kupunguza mzigo wa kazi kwa watumishi waliopo sasa.

Malengo ya Mpango wa Ajira
Kwa mujibu wa Bw. Mkomi, mpango huu una lengo la:
-
Kukidhi mahitaji ya watumishi katika maeneo yenye upungufu mkubwa hasa vijijini.
-
Kuimarisha ubora wa elimu na huduma za afya.
-
Kuwezesha sekta za kilimo, mifugo, na uvuvi kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa taifa.
-
Kuboreshwa kwa usalama wa raia na mali zao kupitia kuajiri askari wapya katika vyombo vya ulinzi.
Serikali imewahimiza Watanzania wenye sifa stahiki kujiandaa kwa mchakato wa maombi ya ajira utakaotangazwa rasmi kupitia Taasisi ya Utumishi wa Umma (PSRS). Aidha, waombaji wanakumbushwa kuwa waangalifu na kuepuka matangazo ya kitapeli, kwani taarifa sahihi za ajira zitatolewa kupitia tovuti rasmi za serikali na vyombo vya habari vinavyoaminika.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako