Haya Hapa Mataifa 9 ya Afrika Yaliyofuzu Kombe la Dunia 2026, Bara la Afrika limepata heshima kubwa baada ya nchi tisa (9) kuthibitisha rasmi kushiriki michuano ya kombe la dunia la FIFA 2026, yatakayofanyika Marekani, Canada na Mexico. Hii ndiyo idadi kubwa zaidi ya timu za Afrika zilizofuzu katika historia ya michuano hiyo tangu kuanzishwa kwake.
Kwa mara ya kwanza katika historia, Afrika itakuwa na uwakilishi mpana zaidi, huku idadi ya timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia ikiongezeka hadi 48. Hatua hii inayapa mataifa mengi fursa ya kuonyesha vipaji vyao na kuongeza ushindani katika bara hilo na kimataifa.
Kati ya mataifa hayo, Morocco inafika na rekodi kali ya kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022, na kuvunja rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya Afrika kutinga hatua hiyo. Senegal na Ghana pia wana historia ya kufanya vyema katika michuano iliyopita, huku Cape Verde na Afrika Kusini zikiendelea kuimarika kimataifa.
Haya Hapa Mataifa 9 ya Afrika Yaliyofuzu Kombe la Dunia 2026

-
๐ช๐ฌ Misri (Egypt)
-
๐ฌ๐ญ Ghana
-
๐ธ๐ณ Senegal
-
๐จ๐ฎ Ivory Coast (Cรดte dโIvoire)
-
๐น๐ณ Tunisia
-
๐จ๐ป Cape Verde
-
๐ฒ๐ฆ Morocco
-
๐ฟ๐ฆ Afrika Kusini (South Africa)
-
๐ฉ๐ฟ Algeria
Afrika inajiandaa kuweka historia katika Kombe la Dunia la 2026, kuonyesha maendeleo makubwa ya kandanda barani. Mataifa haya tisa yana matumaini ya mamilioni ya mashabiki wa Afrika, wanaotarajia ubora, nidhamu, na ushindani wa hali ya juu.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako