Haya Hapa Makundi ya Kombe La Shirikisho CAF 2025/26, Katika droo iliyofanyika leo na kushuudiwa makundi ya CAF Confedaration Cup au Kombe la Shirikisho Afrika kwa msimu mpya wa mashindano wa 2025/2026.
Timu za CECAFA Azam FC na Nairobi United FC zitamenyana katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF la TotalEnergies 2025/2026.
Timu hizo mbili ziliwekwa katika Kundi B wakati wa droo iliyoandaliwa katika Studio ya SuperSport jijini Johannesburg Jumatatu alasiri.
Timu ya Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara chini ya kocha mzoefu, Florent Ibenge imepangwa Kundi B pamoja na Wydad AC (Morocco), AS Maniema Union (DR Congo) na Nairobi United FC.
Singida Black Stars FC, mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame CECAFA pia wamepangwa Kundi C lenye timu za CR Belouizdad (Algeria), Stellenbosch FC (Afrika Kusini) na AS Otoho (Congo Brazzaville).
Droo hiyo iliendeshwa na Mkuu wa Kitengo cha Mashindano cha CAF, Khaled Nassar na kusaidiwa na wachezaji wa zamani wa kimataifa Christopher Katongo (Zambia) na Alex Song (Cameroon).

Mechi za hatua ya makundi zitachezwa kuanzia Novemba 23 hadi Februari mwakani. Zamalek FC ya Misri ilishinda Kombe la Shirikisho la CAF la TotalEnergies 2024/2025/Haya Hapa Makundi ya Kombe La Shirikisho CAF 2025/26.
Haya Hapa Makundi ya Kombe La Shirikisho CAF 2025/26
Group A: USM Alger (Algeria), Djoliba AC de Bamako (Malai), Olympique Club se Safi (Morocco), FS San Pedro
Group B: Wydad AC (Morocco), AS Maniema Union (DR Congo), Azam FC (Tanzania), Nairobi United FC (Kenya)
Group C: CR Belouizdad (Algeria), Stellenbosch FC (South Africa), AS Otoho (Congo Brazzaville), Singida Black Stars FC (Tanzania)
Group D: Zamalek, Al Masry (Egypt), Kaizer Chiefs FC (South Africa), Zesco United FC (Zambia)
CHECK ALSO:
					
							
							







Weka maoni yako