Tarehe Rasmi za AFCON 2027, Kufanyika Juni 19 hadi Julai 18, 2027

Tarehe Rasmi za AFCON 2027, Kufanyika Juni 19 hadi Julai 18, 2027 | Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetangaza tarehe rasmi za kufanyika kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), ambazo kwa mara ya kwanza zitafanyika Afrika Mashariki kupitia ushirikiano wa Kenya, Tanzania na Uganda.

Tarehe Rasmi za AFCON 2027, Kufanyika Juni 19 hadi Julai 18, 2027

Kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa, mashindano hayo yatafanyika kuanzia Juni 19 hadi Julai 18, 2027.

Tangazo hilo limekuja wakati maandalizi ya miundombinu, viwanja na masuala ya kiufundi yakiendelea katika nchi mwenyeji. Tarehe hizi zinatoa muda wa kutosha kwa mataifa shiriki kupanga maandalizi yao, ikiwemo kambi za mazoezi, ratiba za maandalizi na mipango ya usafiri.

Tarehe Rasmi za AFCON 2027, Kufanyika Juni 19 hadi Julai 18, 2027

Mashindano ya AFCON 2027 yanatarajiwa kuvutia umakini mkubwa kutokana na historia yake, maeneo yatakayopokea mechi, na umuhimu wa ukanda wa Afrika Mashariki kuandaa tukio kubwa la kimataifa kwa mara ya kwanza.

Ratiba Rasmi ya Hatua ya Kufuzu

  • Machi 2026 – Mechi za kwanza za kufuzu

  • Septemba 2026 – Mechi za hatua ya makundi zinaendelea

  • Oktoba 2026 – Kamilisho la mechi za makundi

  • Novemba 2026 – Michezo ya mchujo maalum kwa runners-up

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limethibitisha kuwa droo ya kupanga makundi ya hatua ya kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) itafanyika Desemba 19, 2025, katika jiji la Rabat, Morocco.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, droo itaanza saa 18:00 GMT, na itashirikisha mataifa yote yatakayowania kufuzu kuungana na wenyeji wa mashindano, ambao ni Kenya, Tanzania na Uganda.

Wadau wa soka, mashabiki na timu shiriki wanahimizwa kufuatilia taarifa rasmi za CAF kuhusu upangaji wa makundi, viwanja vitakavyopangwa pamoja na ratiba kamili ya michezo itakayothibitishwa katika miezi ijayo.

CHECK ALSO:

  1. Muundo Mpya wa Kufuzu AFCON 2027 Wathibitishwa
  2. Ratiba Rasmi ya Dabi za Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26, Kariakoo na Mzizima
  3. Ratiba Mpya Ya Kariakoo Derby 2025/2026
  4. Simba Yatoa Taarifa ya Majeruhi Wao Kuelekea Mchezo Dhidi ya Petro Atletico