Droo ya Kufuzu AFCON 2027 Kufanyika 19/12/2025 | Droo ya Kufuzu AFCON 2027 Kutangazwa Desemba 19, 2025 Nchini Morocco.
Droo ya Kufuzu AFCON 2027 Kufanyika 19/12/2025
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limethibitisha kuwa droo ya kupanga makundi ya hatua ya kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) itafanyika Desemba 19, 2025, katika jiji la Rabat, Morocco.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, droo itaanza saa 18:00 GMT, na itashirikisha mataifa yote yatakayowania kufuzu kuungana na wenyeji wa mashindano, ambao ni Kenya, Tanzania na Uganda.
Droo hii inatarajiwa kuvuta hisia za wadau wengi kutokana na muundo mpya wa kufuzu, unaojumuisha makundi 13, pamoja na nafasi za ziada kwa timu zilizomaliza nafasi ya pili kupenya kupitia mchujo maalum.

Mataifa shiriki yanatarajiwa kuanza kampeni za kufuzu kuanzia Machi 2026, kabla ya kuhitimisha hatua ya makundi mnamo Oktoba 2026. Mchujo maalum wa runners-up utafanyika Novemba 2026.
Wadau wa soka barani Afrika wanashauriwa kufuatilia kwa karibu matukio ya droo hiyo, ambayo itatoa mwelekeo wa safari ya kila taifa kuelekea mashindano ya AFCON 2027 yatakayofanyika Juni 19 hadi Julai 18, 2027 Afrika Mashariki.
CHECK ALSO:
- Tarehe Rasmi za AFCON 2027, Kufanyika Juni 19 hadi Julai 18, 2027
- Muundo Mpya wa Kufuzu AFCON 2027 Wathibitishwa
- Ratiba Rasmi ya Dabi za Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26, Kariakoo na Mzizima
- Ratiba Mpya Ya Kariakoo Derby 2025/2026
- Simba Yatoa Taarifa ya Majeruhi Wao Kuelekea Mchezo Dhidi ya Petro Atletico








Weka maoni yako