Nafasi Mpya za Kazi SHDEPHA+ November 2024 | Mwisho 18 November 2024

Nafasi Mpya za Kazi SHDEPHA+ November 2024 | Mwisho 18 November 2024

Kampuni ya SHDEPHA+ imetangaza nafasi mpya ya kazi ya Procurement Officer ambaye atakuwa akitimiza majukumu mbalimbali ya ununuzi na usimamizi wa ugavi kwa malengo ya kuimarisha ufanisi wa shirika.

Nafasi hii ni muhimu katika kusaidia utekelezaji wa malengo ya SHDEPHA+ katika kutoa msaada kwa makundi maalum yanayohitaji msaada wa kiuchumi na kijamii, ikiwa ni pamoja na watu wanaoishi na VVU na makundi mengine yaliyo hatarini.

SHDEPHA+ ni shirika la kitaifa lisilo la kiserikali lililoanzishwa mwaka 1994, likiwa na lengo la kupambana na kuenea kwa VVU/UKIMWI na kusaidia watu wanaoishi na hali hii. Hadi sasa, shirika limepanua wigo wake kwa kushirikiana na wafadhili wa kitaifa na kimataifa pamoja na serikali katika ngazi zote kwa ajili ya kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

SHDEPHA+ lina makao makuu yake katika Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga, na linafanya kazi katika mikoa tisa Tanzania Bara, ambapo linahudumia makundi mbalimbali kama wanawake, watoto, vijana, na watu wenye mahitaji maalum.

Nafasi Mpya za Kazi SHDEPHA+ November 2024 | Mwisho 18 November 2024

Taarifa za Nafasi ya Kazi: Procurement Officer

  • Nafasi: Procurement Officer (Mmoja)
  • Mahali: Kahama, Shinyanga
  • Ripoti kwa: Meneja wa Fedha
  • Mkataba: Mwaka 1 (Unaoweza kuongezwa)

Majukumu na Wajibu

Mtu atakayechaguliwa atakuwa na majukumu yafuatayo:

  • Kufanya tathmini ya wazabuni kwa kuzingatia ubora, gharama, na uhakika wa huduma zinazotolewa.
  • Kujadiliana na wazabuni kuhusu masharti ya mikataba ili kupata bei na masharti yenye manufaa kwa shirika.
  • Kusimamia wafanyakazi na shughuli zote za kitengo cha ununuzi ili kuhakikisha ufanisi.
  • Kushirikiana na wadau wa ndani ili kutambua mahitaji ya ununuzi na kutoa msaada wa kiufundi.
  • Kudumisha mahusiano mazuri na wazabuni kwa kuhakikisha uwasilishaji wa bidhaa na huduma kwa wakati.
  • Kusimamia mchakato mzima wa ununuzi kuanzia maombi hadi uwasilishaji wa bidhaa, pamoja na kufuatilia na kushughulikia changamoto zozote zinazoibuka.
  • Kufanya tathmini za mara kwa mara za wazabuni ili kuhakikisha wanakidhi vigezo vya mikataba.
  • Kubuni mbinu za kupunguza gharama na kuboresha michakato ndani ya kitengo cha ununuzi.
  • Kuhakikisha kuwa shughuli zote zinafuata sera, taratibu, na kanuni za shirika.

Vigezo na Sifa za Mwombaji

  • Shahada ya Ununuzi na Usimamizi wa Ugavi, Usimamizi wa Ugavi, au fani inayofanana.
  • Uzoefu wa angalau miaka 1-2 katika ununuzi, ugavi, au usimamizi wa ugavi, hasa katika mashirika yasiyo ya kiserikali.
  • Uwezo wa kufanya majadiliano yenye lengo la kupunguza gharama na kupata masharti mazuri.
  • Uwezo mzuri wa uchambuzi na utatuzi wa matatizo.
  • Ujuzi wa kutumia programu za ununuzi na zana za kiufundi.
  • Uwezo mzuri wa kuwasiliana na kujenga mahusiano na wadau wa ndani na wazabuni.
  • Cheti cha taaluma kama Certified Procurement and Supply Professional (CPSP-T) au MCIPS ni nyongeza nzuri.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Wale wanaokidhi vigezo vilivyoainishwa na wana nia ya nafasi hii wanatakiwa kutuma barua ya maombi na wasifu (CV) kwa kuunganisha kwenye faili moja, wakieleza mwajiri wao wa sasa au wa hivi karibuni, nafasi wanayoshikilia, namba ya simu, pamoja na majina na anwani za marejeo watatu. Mwombaji pia anatakiwa kujaza fomu inayopatikana kupitia kiungo cha fomu ya maombi hapa https://forms.gle/QBJbt9NBrtetx1Pf6

Mwisho wa Kutuma Maombi: Maombi yote lazima yawasilishwe kabla ya saa 11:00 jioni, Jumatatu, tarehe 18 Novemba 2024. Mwombaji anatakiwa kutaja nafasi ya kazi anayoomba kwenye kichwa cha barua pepe.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Nafasi Mpya za Kazi Twiga Cement Limited November 2024
  2. Nafasi Mpya za kazi Heritage Insurance Tanzania |Mwisho wa Kutuma Maombi 10 November 2024
  3. Nafasi Mpya Ya Ajira kampuni ya Ciheb Tanzania November 2024
  4. Nafasi Mpya za Kazi Cococola Kwanza November 2024
  5. Nafasi Mpya za Kazi Kampuni ya SNV Tanzania October 2024