Mgogoro Waibuka, Mbappé Adai €253 Milioni, PSG Wataka €180 Milioni

Mgogoro Waibuka, Mbappé Adai €253 Milioni, PSG Wataka €180 Milioni | Mgogoro Mpya Kati ya Mbappé na PSG Wafichua Tuhuma Nzito za Mkataba.

Mgogoro Waibuka, Mbappé Adai €253 Milioni, PSG Wataka €180 Milioni

Taarifa kutoka Le Parisien zimeibua mzozo mkubwa kati ya Kylian Mbappé na klabu yake ya zamani ya Paris Saint-Germain (PSG). Mzozo huu wa kisheria unaonyesha tofauti kubwa za madai ya kifedha kati ya pande hizo mbili, huku kila upande ukisisitiza madai yake kwa msimamo mkali.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Mbappé anadai PSG imemkopa jumla ya €253 milioni, akieleza kuwa kiasi hicho kinajumuisha mishahara na malipo mengine ambayo anahisi hakuyapata kama ilivyokubaliwa katika mkataba wake.

Hata hivyo, PSG imejibu kwa msimamo mkali. Klabu hiyo inamtaka mshambuliaji huyo alipe €180 milioni, ikisisitiza kuwa ni Mbappé ndiye anayewadaiwa. PSG inadai kuwa wachezaji na klabu wanapaswa kuheshimu makubaliano yote ya kandarasi bila kuyachagua.

Tuhuma za Kuficha Taarifa za Uhamisho

Katika taarifa hiyo hiyo, PSG imefungua ukurasa mpya wa tuhuma nzito. Klabu hiyo inasisitiza kuwa Mbappé alificha mazungumzo yake ya kujiunga na Real Madrid.

Mgogoro Waibuka, Mbappé Adai €253 Milioni, PSG Wataka €180 Milioni

Ripoti inaeleza kuwa:

  • Mbappé aliripotiwa kuanza mawasiliano na Real Madrid kati ya Julai 2022 na Agosti 2023,
  • PSG inadai hakutoa taarifa hiyo kama inavyotakiwa na kanuni za mikataba,
  • Hatua hiyo ilifanya klabu ishindwe kumuuza kabla ya mkataba wake kuisha,
  • Na hatimaye, mchezaji huyo akaondoka bure, bila malipo yoyote kwa klabu.

Kwa hoja ya PSG, kitendo hicho kilisababisha hasara kubwa ya kifedha kwa klabu, na ndio msingi wa madai yao ya fidia.

CHECK ALSO:

  1. TFF Awards 2025, Tuzo za Soka Tanzania Kufanyika Desemba 05 2025
  2. Yanga Kuzindua Jezi Mpya za CAF Champions League Novemba 20, 2025
  3. Dirisha Dogo la Usajili 2025/2026 Litafunguliwa Januari 1-30, 2026
  4. Droo ya Kufuzu AFCON 2027 Kufanyika 19/12/2025