Al Hilal Omdurman Yaanza Hatua ya Makundi CAFCL Kwa Ushindi wa 2-1 Dhidi ya MC Alger Kigali | Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika imeanza kwa kasi, huku Al Hilal Omdurman ya Sudan ikipata ushindi muhimu wa 2-1 dhidi ya MC Alger ya Algeria katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali, Rwanda. Ushindi huu unaiweka Al Hilal katika nafasi nzuri ya kuanza kampeni za makundi kwa kujiamini.
Mchezo ulianza kwa tahadhari kubwa kutoka pande zote mbili, lakini Al Hilal ilionyesha kuwa na mpango imara licha ya MC Alger kuwa na kikosi kilicho chini ya kocha mwenye uzoefu mkubwa barani Afrika — aliyewahi kuinoa Mamelodi Sundowns na Wydad Casablanca.
Al Hilal Omdurman Yaanza Hatua ya Makundi CAFCL Kwa Ushindi
Al Hilal ilipata bao lake la kwanza dakika ya 45+1, kupitia Omer, jambo lililowapa nguvu kabla ya kwenda mapumziko. MC Alger ilisawazisha dakika ya 53, kupitia kwa Karshom, ambaye alijifunga kwa bahati mbaya.
Hata hivyo, Al Hilal haikukata tamaa. Dakika ya 75, Abdelrahman aliipatia timu yake bao la pili na la ushindi, lililozima matumaini ya MC Alger kurejea mchezoni.

Dakika za mwisho za mchezo ziliendelea kuwa ngumu kwa Al Hilal baada ya Alhassan kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 87, lakini waliweza kuhimili mashambulizi hadi filimbi ya mwisho.
MC Alger, licha ya kupoteza mchezo wao wa kwanza, wanaendelea na maandalizi ya kukabiliana na Mamelodi Sundowns wiki ijayo. Kocha wao, ambaye amewahi kuinoa klabu hiyo ya Afrika Kusini, anakabiliwa na shinikizo la kutafuta ushindi dhidi ya waajiri wake wa zamani.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia ya kocha huyo na timu anayoenda kukutana nayo/Al Hilal Omdurman Yaanza Hatua ya Makundi CAFCL Kwa Ushindi.
Ushindi wa Al Hilal Omdurman umefungua kwa nguvu hatua ya makundi ya CAF Champions League msimu huu. Kwa upande mwingine, MC Alger italazimika kurekebisha makosa ili kujiweka vizuri katika michezo ijayo. Timu zote zinasalia na nafasi ya kufanya vizuri, lakini zinahitaji nidhamu ya kimchezo na maandalizi ya kina katika hatua zinazofuata.
CHECK ALSO:








Weka maoni yako