Orodha ya Wafungaji Bora CAF Champions League 2025/26: Trézéguet Aongoza Mbio za Kiatu cha Dhahabu.
Michuano ya CAF Champions League inaendelea kupamba moto, huku ushindani wa Kiatu cha Dhahabu (Golden Boot) ukizidi kuwa mkali kadri hatua ya makundi inavyoendelea. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha wachezaji kadhaa wakijitokeza kwa ubora mkubwa katika ufungaji.
Kwa sasa, mshambuliaji wa Al Ahly SC, Mahmoud Trézéguet, anaongoza chati ya wafungaji bora baada ya kufunga mabao matano.
Orodha ya Wafungaji Bora CAF Champions League 2025/26
Hali ya wafungaji bora wa CAF Champions League kwa sasa iko kama ifuatavyo:
-
Mahmoud Trézéguet (Al Ahly SC) – Mabao 5
-
Abdelrazig Omer (Al-Hilal SC) – Mabao 4
-
Ahmed Atef (Pyramids FC) – Mabao 3
Aidha, wachezaji wafuatao wana mabao mawili kila mmoja:

-
Kashala Ramos – FC Saint-Éloi Lupopo
-
Mounir Chouiar – RS Berkane
-
Nuno Santos – Mamelodi Sundowns
-
Taddeus Nkeng – Stade Malien
Orodha hii inaonyesha usawa mkubwa wa ushindani, huku wachezaji kutoka ligi na klabu tofauti wakionesha uwezo wao barani Afrika.
CHECK ALSO:






Weka maoni yako