Adel Amrouche Atangazwa Kuwa Kocha Mpya wa Rwanda

Adel Amrouche Atangazwa Kuwa Kocha Mpya wa Rwanda | Adel Amrouche Atua Rwanda Kama Kocha Mpya wa Amavubi Licha ya Kuwa na Mkataba na TFF.

Adel Amrouche Atangazwa Kuwa Kocha Mpya wa Rwanda

Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Adel Amrouche ametangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, jambo ambalo linazua mjadala mkubwa kutokana na ukweli kuwa bado ana mkataba na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unaotarajiwa kumalizika mwakani.

Tangazo hilo lilitolewa na Shirikisho la Soka la Rwanda (FERWAFA), likieleza kuwa Amrouche atasaidiwa na makocha wawili wazawa; Erick Nshimiyimana, ambaye atakuwa kocha msaidizi wa kwanza, na Dk Carolin Braun, ambaye atachukua nafasi ya msaidizi wa pili.

Adel Amrouche Atangazwa Kuwa Kocha Mpya wa Rwanda
Adel Amrouche Atangazwa Kuwa Kocha Mpya wa Rwanda

Hadithi ya Amrouche na mivutano yake na CAF

Uamuzi huu unakuja wiki chache baada ya Amrouche kushinda kesi dhidi ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ambapo alitakiwa kulipwa fidia ya mzozo wake wa awali. Ushindi huo uliongeza uzito kwa jina lake katika soka la Afrika na sasa amepata kibarua kipya Amavubi.

Sina uhakika na mkataba wake na TFF.

Pamoja na kwamba timu ya Taifa ya Rwanda imempa Amrouche majukumu mapya, bado haijafahamika suala la mkataba wake na TFF litashughulikiwa vipi. Hili linaweza kusababisha mgogoro wa kisheria kati yake na Shirikisho la Soka Tanzania, iwapo hakutakuwa na makubaliano rasmi ya kusitisha mkataba wake.

TFF bado haijatoa tamko rasmi kuhusu suala hilo, lakini kitendo cha Amrouche kinaweza kuathiri mustakabali wa Taifa Stars, hasa ikizingatiwa kuwa bado ana muda wa kuitumikia timu hiyo.

CHECK ALSO: