Takwimu za Mechi ya Simba na Yanga LIGI KUU

Takwimu za Mechi ya Simba na Yanga LIGI KUU | Takwimu za Yanga vs Simba Mechi Zilizopita Tangu Msimu wa 2017/18. Mechi kati ya Simba SC na Yanga SC ni moja ya mechi kubwa na ya kusisimua katika historia ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Upinzani kati ya wababe hao wawili unaonekana kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka kwani kila mechi ina hadithi yake.

Takwimu za Mechi ya Simba na Yanga LIGI KUU

Rekodi ya mechi zilizopita

Tangu msimu wa 2017/18, Simba na Yanga zimekutana mara 14 kwenye Ligi Kuu, Yanga ikishinda mara 5, Simba mara 3 na mechi 6 zikimalizika kwa sare. Hizi hapa rekodi za mechi hizo:

04/29/2018: Simba 1-0 Yanga
09/30/2018: Simba 0-0 Yanga
02/16/2019: Yanga 0-1 Simba
04/01/2020: Simba 2-2 Yanga
08/03/2020: Yanga 1-0 Simba
07/11/2020: Yanga 1-1 Simba
03/07/2021: Simba 0-1 Yanga
11/12/2021: Simba 0-0 Yanga
04/30/2022: Yanga 0-0 Simba
10/23/2022: Yanga 1-1 Simba
04/16/2023: Simba 2-0 Yanga
11/05/2023: Simba 1-5 Yanga
04/20/2024: Yanga 2-1 Simba
10/19/2024: Simba 0-1 Yanga

Takwimu za Mechi ya Simba na Yanga LIGI KUU
Takwimu za Mechi ya Simba na Yanga LIGI KUU

Uchambuzi wa Rekodi

  1. Yanga ina rekodi nzuri zaidi: ikiwa imeshinda mara tano dhidi ya watani wake wa jadi, Yanga imeonyesha ubabe katika michezo ya ligi tangu msimu wa 2017/18.
  2. Simba imefanikiwa kushinda mara tatu: ushindi wao wa mwisho ulikuwa Aprili 16, 2023, kwa mabao 2-0.
    Mechi nyingi huisha kwa sare: kati ya mechi 14, 6 zilimalizika kwa sare, kuonyesha ugumu wa mashindano haya.
  3. Ushindi mkubwa zaidi: Yanga ilishinda 5-1 dhidi ya Simba Novemba 5, 2023, ikionyesha kiwango bora zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa kuzingatia rekodi za mechi hizo, Yanga inaonekana kuwa na rekodi nzuri zaidi dhidi ya Simba kwenye Ligi Kuu tangu msimu wa 2017/18. Hata hivyo, kila mechi ya Kariakoo derby ina matokeo yasiyotabirika na kila timu inajitahidi kutawala soka la Tanzania.

Mashabiki sasa wanatazamia mechi zijazo kuona iwapo Simba wataweza kubadili historia au Yanga kuendeleza ubabe wao/Takwimu za Mechi ya Simba na Yanga LIGI KUU.

CHECK ALSO: