Ahmed Arajiga Kuchezesha Kariakoo Derby

Ahmed Arajiga Kuchezesha Kariakoo Derby | Historia Inaipa Yanga Nafasi Kubwa?. Baada ya Kamati ya Waamuzi wa Tanzania kumteua Ahmed Arajiga wa Manyara kuchezesha mchezo wa Kariakoo derby kati ya Simba SC na Yanga SC Machi 8, 2025, mashabiki wa soka wanajiuliza iwapo rekodi yake katika mechi za jadi inaweza kuwa kielelezo cha matokeo yajayo.

Ahmed Arajiga Kuchezesha Kariakoo Derby

Rekodi ya Ahmed Arajiga katika michezo ya kiasili

Katika mechi nne alizocheza kati ya timu hizi mbili, Simba SC imefanikiwa kushinda mara moja tu, huku Yanga SC ikitawala kwa ushindi huo mara tatu.

Matokeo ya Zamani Chini ya Mwamuzi Ahmed Arajiga:

  1. Julai 25, 2021Simba 1-0 Yanga (Fainali ya FA Cup)
    • Bao pekee lilifungwa na Taddeo Lwanga (Uganda).
  2. Nusu Fainali FA CupYanga 1-0 Simba (CCM Kirumba)
    • Feisal Salum alifunga bao la ushindi.
  3. Novemba 5, 2023Yanga 5-1 Simba (Ligi Kuu Tanzania Bara)
    • Yanga ilipata ushindi mnono kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
  4. Aprili 20, 2024Yanga 2-1 Simba (Ligi Kuu Tanzania Bara)
    • Mechi nyingine ya ligi kuu iliyochezwa Benjamin Mkapa ilimalizika kwa ushindi wa Yanga.
Ahmed Arajiga Kuchezesha Kariakoo Derby
Ahmed Arajiga Kuchezesha Kariakoo Derby

Je, Simba itabadilisha historia?

Kwa kuangalia rekodi hii, Yanga SC inaonekana kuwa na nguvu zaidi wakati Ahmed Arajiga akiwa madarakani. Walakini, historia haimaanishi kuwa matokeo yatakuwa sawa kila wakati/Ahmed Arajiga Kuchezesha Kariakoo Derby.

Simba SC itashuka uwanjani ikiwa na nia ya kulipiza kisasi hasa baada ya kipigo cha mabao 5-1 mwaka 2023. Wakati huo huo Yanga SC watataka kuendeleza ubabe wao na kuthibitisha kwa mara nyingine kuwa wao ndio mabingwa wa soka la Tanzania.

Mashabiki wa soka wanasubiri kuona iwapo Ahmed Arajiga ataongeza mechi nyingine kwenye rekodi nzuri ya Yanga, au Simba itavunja mwiko huo na kuambulia ushindi wa pili chini ya mwamuzi.

CHECK ALSO: