Alama Za Ufaulu Kidato Cha Nne | Madaraja ya Ufaulu O-Level Shule za Sekondari
Alama za ufaulu kwa kidato cha nne nchini Tanzania ni mfumo maalumu unaotumiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika kutathmini ufanisi wa wanafunzi katika mitihani ya taifa. Mfumo huu ni wa viwango maalum (grading system) unaoeleza wazi kiwango cha ufahamu, maarifa, na ujuzi wa mwanafunzi katika masomo anayoyafanyia mtihani.
Pia, viwango hivi vinasaidia katika kutoa mwongozo muhimu kwa wanafunzi, wazazi, na taasisi za elimu kuhusu maendeleo ya wanafunzi na hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa ajili ya kujiendeleza zaidi kitaaluma. Katika makala hii, tutachambua kwa kina maana ya viwango vya ufaulu kwa kidato cha nne na namna matokeo haya yanavyotunukiwa.
Muundo wa Alama za Ufaulu Kidato cha Nne
Baraza la mitihani Tanzania, NECTA hutumia mfumo wa alama kuonyesha ufaulu wa mwanafunzi kwa kila somo alilofanyia mtihani.
Alama hizi hupangwa kwenye viwango vitano vya madaraja kuanzia Daraja la Kwanza (Division I) hadi sifuri (Division 0). Kila daraja lina alama za jumla zinazopatikana kwa kujumlisha pointi za alama za masomo binafsi kama ifuatavyo:
Madaraja ya Ufaulu na Maelezo
- Division I: Daraja la Kwanza linajumuisha alama za jumla 7-17. Hili ni daraja la juu zaidi linaloashiria uwezo mzuri sana wa kitaaluma na ufahamu wa kina wa masomo.
- Division II: Hii ni kwa alama za jumla 18-21, ikionyesha uwezo mzuri wa kitaaluma na ufahamu mzuri wa mada.
- Division III: Alama za jumla kati ya 22-25. Daraja hili linaashiria uwezo wa wastani lakini bado ni mzuri kwa masomo.
- Division IV: Kwa alama 26-33, mwanafunzi amefaulu kwa kiwango cha kuridhisha lakini anahitaji kuboresha katika maeneo fulani.
- Division 0: Hili ni daraja la sifuri lenye alama za jumla 34-35, na linaonyesha kuwa mwanafunzi hajapata ufaulu wa kutosha kuendelea na masomo ya juu zaidi.
Maana ya Alama Kila Somo
Katika kuonesha uwezo aloonesha mwanafunzi katika mtihani fulani, kila somo hupangiwa alama ya ufaulu kulingana na pointi ambazo mwanafunzi amepata katika mtihani wa somo usika. Alama hizo hupangwa kulingana na viwango maalumu vilivyowekwa na NECTA na i navyo onekana katika hedwahi hapa chini,
Gredi | Alama | Pointi za Gredi | Maelezo |
A | 75-100 | 1 | Bora sana (Excellent) |
B | 65-74 | 2 | Vizuri sana (Very Good) |
C | 45-64 | 3 | Vizuri (Good) |
D | 30-44 | 4 | Inaridhisha (Satisfactory) |
F | 0-29 | 5 | Feli (Fail) |
Alama hizi zinaonyesha kiwango cha ufahamu wa mwanafunzi katika somo husika. Kwa mfano, mwanafunzi aliyepata daraja la A ana uelewa mkubwa wa somo, wakati daraja F linaashiria kuwa mwanafunzi hajaelewa kikamilifu.
Vigezo vya Kupata Daraja la Ufaulu
Kwa mwanafunzi anayefanya masomo yasiyopungua saba, NECTA hutunuku ufaulu kwa jumla ya alama (total points).
Ikiwa mwanafunzi anafanya masomo chini ya saba, anahesabiwa kuwa amefaulu kwa kiwango cha chini zaidi endapo atapata alama ya D katika masomo mawili au zaidi, au alama moja katika A, B, au C.
Hii inampa mwanafunzi fursa ya kupata angalau daraja la nne (Division IV), ambalo ni kigezo cha msingi cha ufaulu.
Kwa upande wa wanafunzi wa kidato cha sita, endapo watafanya masomo chini ya matatu, wanaweza kupatiwa daraja la nne ikiwa watafaulu masomo mawili katika daraja S, au alama moja katika A, B, C, D, au E.
Umuhimu wa Matokeo ya Kidato cha Nne kwa Maendeleo ya Kitaaluma
Matokeo ya kidato cha nne ni hatua muhimu katika safari ya elimu ya mwanafunzi. Aina na daraja la ufaulu analopata mwanafunzi huweza kuathiri nafasi zake za kuendelea na elimu ya juu, kupata nafasi za masomo ya ufundi au vyuo vikuu, au hata fursa za ajira kwa waliohitimu elimu ya msingi ya sekondari. Katika muktadha huu, mfumo wa madaraja unawapa wanafunzi picha halisi ya uwezo wao, maeneo ya kuboresha, na fursa zinazopatikana kwa kila hatua ya ufaulu.
Jinsi ya Kuhesabu Division ya Matokeo ya Kidato cha Nne
Ili kupata daraja (division) ya matokeo ya mwanafunzi wa kidato cha nne, NECTA hujumlisha pointi za kila somo alilofanya mwanafunzi. Mfano:
- Division I: Jumla ya pointi 7-17
- Division II: Jumla ya pointi 18-21
- Division III: Jumla ya pointi 22-25
- Division IV: Jumla ya pointi 26-33
- Division 0: Jumla ya pointi 34-35
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka maoni yako