Azam FC Kuzindua Jezi Mpya Msimu wa 2025/2026 Leo

Azam FC Kuzindua Jezi Mpya Msimu wa 2025/2026 Leo: Azam FC imetangaza rasmi kuzindua jezi zake mpya kwa msimu wa 2025/2026. Uzinduzi huo utafanyika leo Jumapili kwenye Ukumbi wa Maonesho wa Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Azam FC Kuzindua Jezi Mpya Msimu wa 2025/2026 Leo

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja Masoko na Mauzo wa klabu hiyo Bw.Tunga Ally, hafla hiyo ya uzinduzi inatarajiwa kuwa ya kipekee na yenye mvuto mkubwa kwa mashabiki wa soka nchini.

Azam FC Kuzindua Jezi Mpya Msimu wa 2025/2026 Leo
Azam FC Kuzindua Jezi Mpya Msimu wa 2025/2026 Leo

Katika hotuba yake kwa vyombo vya habari, Mheshimiwa Tunga alisema:

“Tunawaalika mashabiki wote wa Azam FC na wapenda soka kwa ujumla, waje kuona mtoko wa kuvuruga watu. Jezi hizi mpya si tu ni za kisasa bali pia zimebeba ubora, hadhi, na historia ya klabu yetu.”

Uzinduzi huu ni sehemu ya maandalizi ya klabu kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC na mashindano mengine ya kitaifa na kimataifa. Azam FC imekuwa ikifanya kazi ya kuongoza katika kuboresha hadhi ya klabu kupitia bidhaa rasmi kama jezi, mavazi na vifaa vingine vya mashabiki.

Wataalamu wa masuala ya masoko wanabainisha kuwa hatua hizi zinaimarisha uhusiano kati ya klabu na mashabiki wake, huku pia zikichangia mapato yake ya ndani.

CHECK ALSO:

  1. Best Football Clubs In Africa 2025/2026 CAF Club Ranking
  2. Yanga Yatoa Msimamo wa Aziz Ki na Kufichua Ujio wa Kocha Mpya
  3. CAF Yaongeza Zawadi WAFCON 2025, Mshindi Kupata Dola Milioni 1
  4. Fountain Gate Yaichapa Stand United 3-1 Kwenye Playoff, Marudiano Julai 8