Azam Yaaga Mashindano ya Muungano Cup 2025 Baada ya Kipigo Kutoka JKU | Katika muendelezo wa michuano ya Kombe la Muungano 2025, Azam FC ilitolewa mapema baada ya kufungwa na JKU SC kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa leo.
Azam Yaaga Mashindano ya Muungano Cup 2025 Baada ya Kipigo Kutoka JKU
Matokeo haya yamewafanya mashabiki wa Azam FC kuwa na majonzi makubwa, huku timu yao ikipoteza nafasi ya kusonga mbele katika mashindano hayo muhimu.
Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Gomba ulivutia umati mkubwa wa watu, ambapo JKU SC walionyesha umahiri mkubwa na dhamira ya kusonga mbele. Ushindi huu umeihakikishia JKU kutinga hatua inayofuata ya mashindano hayo.

Kwa sasa JKU SC inasubiri mshindi kati ya Zimamoto na Yanga SC zinazotarajiwa kumenyana kesho kwenye uwanja huo huo wa Gomba. Mshindi wa mechi hiyo atakutana na JKU SC katika nusu fainali.
Michuano ya Kombe la Muungano 2025 inaendelea kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka, na mchuano huo mkali unatarajiwa kuimarika zaidi kadri hatua ya mtoano ikiendelea.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako