Aziz Ki Afanya Mazoezi na Wenzake, Uwezekano Kucheza Kariakoo Derby Bado ni 50/50
Kiungo nyota wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki ameungana na wenzake mazoezini kujiandaa na mchezo wa Kariakoo Derby dhidi ya Simba SC.
Aziz Ki alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya nyonga na hivyo kuweka ushiriki wake katika mechi hiyo muhimu ya ligi kuu ya Tanzania bara mashakani. Hata hivyo Kocha wa Yanga SC Miloud Hamdi amesema bado kuna asilimia 50/50 ya mchezaji huyo kucheza kesho.

Mashabiki wa Yanga SC wanatumai kuwa nyota huyo ataweza kushiriki katika pambano dhidi ya wapinzani wao wa jadi Simba SC, litakalopigwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 13:00.
ANGALIA PIA:








Weka maoni yako