Azizi Ki Kucheza Mchezo Wake wa Mwisho Yanga SC Leo Dhidi ya JKT Tanzania

Azizi Ki Kucheza Mchezo Wake wa Mwisho Yanga SC Leo Dhidi ya JKT Tanzania – Apewa Ukapteni wa Heshima

Azizi Ki Kucheza Mchezo Wake wa Mwisho Yanga SC Leo Dhidi ya JKT Tanzania

Kiungo mahiri wa Klabu ya Yanga SC, Stephane Aziz Ki, anatarajiwa kucheza mchezo wake wa mwisho leo jioni wakati timu yake itakapomenyana na JKT Tanzania katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya CRDB Bank CUP.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu, Azizi Ki ataiongoza Yanga SC kama nahodha katika mchezo huo wa leo ikiwa ni sehemu ya heshima maalumu ya kumuaga kiungwana kabla ya kuondoka rasmi ndani ya kikosi cha Wananchi. Hatua hiyo inalenga kumuenzi kutokana na mchango wake mkubwa ndani ya timu tangu alipojiunga.

Baada ya mchezo wa leo dhidi ya JKT Tanzania, Azizi Ki hataendelea kuonekana katika michezo mingine iliyosalia ya klabu hiyo msimu huu, hali inayoashiria kuwa huu ndio mwisho wa safari yake rasmi akiwa na jezi ya Yanga SC.

Azizi Ki Kucheza Mchezo Wake wa Mwisho Yanga SC Leo Dhidi ya JKT Tanzania
Azizi Ki Kucheza Mchezo Wake wa Mwisho Yanga SC Leo Dhidi ya JKT Tanzania

Kuelekea michuano ya kombe la vilabu duniani Wydad CA wataanza kambi rasmi mwishoni mwa mwezi huu. Hivyo sajili wanazotarajia kuzikamilisha akiwemo Stephanie Aziz Ki zitajiunga kikosini mapema

Mashabiki wa Yanga na wapenzi wa soka kwa ujumla wanahimizwa kufuatilia kwa karibu mchezo huu muhimu, ambao si tu unaamua tiketi ya kuingia fainali ya CRDB CUP, bali pia unatoa fursa ya kumuaga rasmi mchezaji muhimu ambaye amekuwa sehemu ya mafanikio ya klabu katika misimu ya hivi karibuni.

CHECK ALSO: