CAF Champions League 2024/25 Fainali Pyramids na Mamelodi Sundowns: Klabu ya Pyramids FC ya Misri imeweka historia ya kufuzu kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kwa mara ya kwanza, kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Orlando Pirates katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali.
CAF Champions League 2024/25 Fainali Pyramids na Mamelodi Sundowns
Mechi hiyo ya kusisimua iliisha kwa jumla ya mabao 3-2, huku mshambuliaji tegemeo wa Pyramids, Fiston Mayele akifunga mabao mawili muhimu, likiwemo la ushindi wa dakika ya 87, na kuipa Pyramids tiketi ya kutinga fainali ya kihistoria.
Kwa matokeo haya, Pyramids FC sasa itamenyana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika fainali ya 2024/25. Mamelodi ilifuzu kwa kutumia faida ya mabao ya ugenini baada ya kutoka sare ya 1-1 kwa jumla ya mabingwa Al Ahly.

Ratiba ya Fainali ya CAFCL 2024/25:
🏟 Mkondo wa Kwanza: Mei 25, 2025 – Afrika Kusini
🏟 Mkondo wa Pili: Juni 1, 2025 – Misri
Mashabiki wa soka barani Afrika sasa wanatazama kwa hamu mechi ya fainali, wakijiuliza:
Je, Mamelodi Sundowns watatwaa taji kwa mara nyingine?
Au Pyramids FC watatwaa taji lao la kwanza kabisa?
Kwa viwango vilivyooneshwa na timu zote mbili, mashindano haya yanatarajiwa kuhitimishwa kwa fainali yenye ushindani mkubwa na burudani ya hali ya juu.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako