CAF CHAN 2024 Mechi ya Ufunguzi Kupigwa Tanzania na Fainali Kenya

CAF CHAN 2024 Mechi ya Ufunguzi Kupigwa Tanzania na Fainali Kenya | Tanzania itakuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguzi, Mechi ya fainali kuchezeka Kenya, na Uganda mechi ya mshindi wa tatu.

Michuano ya Mataifa ya Afrika ya 2024 (CAF CHAN) itaandaliwa kwa pamoja na mataifa matatu ya Afrika Mashariki: Tanzania, Kenya na Uganda.

Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano ya CAF yanafanyika katika mfumo wa kanda ya pamoja, kuonyesha mshikamano na maendeleo ya soka katika ukanda huu.

CAF CHAN 2024 Mechi ya Ufunguzi Kupigwa Tanzania na Fainali Kenya

  • Mechi ya Ufunguzi itapigwa Dar es Salaam, Tanzania, siku ya Jumamosi, tarehe 2 Agosti 2025. Tanzania imepewa heshima ya kufungua mashindano kutokana na miundombinu imara na historia ya mashindano ya kimataifa.

CAF CHAN 2024 Mechi ya Ufunguzi Kupigwa Tanzania na Fainali Kenya
CAF CHAN 2024 Mechi ya Ufunguzi Kupigwa Tanzania na Fainali Kenya
  • Mechi ya Fainali itafanyika Nairobi, Kenya, siku ya Jumamosi, tarehe 30 Agosti 2025. Kenya itaandaa fainali hiyo ambayo itaamua bingwa wa CHAN 2024, tukio linalotarajiwa kuvuta mashabiki kutoka ndani na nje ya Afrika.

  • Mechi ya Kusaka Nafasi ya Tatu (Third Place Match) utapigwa Kampala, Uganda, katika hatua ya awali ya wiki ya mwisho ya mashindano haya. Uganda itakuwa mwenyeji wa pambano hili muhimu kwa timu zitakazoshindwa katika hatua ya nusu fainali.

Uamuzi wa kugawanya mechi kuu kati ya nchi tatu unalenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda, kukuza utalii wa michezo, na kuwapa mashabiki kutoka mikoa mbalimbali fursa ya kushuhudia soka/CAF CHAN 2024 Mechi ya Ufunguzi Kupigwa Tanzania na Fainali Kenya.

Mashabiki wanashauriwa kushauriana na ratiba kamili ya mashindano kupitia tovuti rasmi za CAF na vyombo vya habari vilivyoidhinishwa. Timu shiriki zinapaswa kuhakikisha zinafanya maandalizi ya mapema ya usafiri na malazi, kwani michuano hiyo itahusisha safari za kimataifa.

Michuano ya CAF CHAN inawapa wachezaji wa ndani fursa ya kuonyesha vipaji vyao bila kushindana na wachezaji wa kigeni. Kwa hivyo, CAF CHAN 2024 inatarajiwa kuwa jukwaa muhimu kwa talanta chipukizi kujiimarisha kimataifa.

CHECK ALSO:

  1. Pilato wa Simba Beida Apangwa Kuchezesha Mechi ya FIFA Club World Cup 2025
  2. Timu za Afrika Katika Raundi ya 1 Kombe la Dunia la Vilabu FIFA 2025
  3. Ratiba ya Raundi ya Awali Mashindano CAF 2025/26
  4. FIFA Yairuhusu Congo-Brazzaville Kuendelea na Mechi za Kufuzu Kombe la Dunia 2026