CAF Confederation Cup 2025/26 Azam FC, Singida Black Stars na KMKM: Wawakilishi wa Tanzania Bara na Zanzibar katika msimu wa 2025/26 CAF Confederation Cup (CAFCC) wametangaza wapinzani wao katika hatua ya awali ya michuano hiyo kufuatia droo rasmi.
CAF Confederation Cup 2025/26 Azam FC, Singida Black Stars na KMKM
Azam FC, moja ya timu zilizotamba zaidi kwenye Ligi Kuu Bara, itamenyana na Al Merriekh Bentiu ya Sudan Kusini. Wakati huohuo, Singida Black Stars itamenyana na Rayon Sports ya Rwanda. Wawakilishi wa Zanzibar, KMKM, watamenyana na AS Sport ya Djibouti.
Kwa mujibu wa kalenda ya CAF, mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa ugenini kati ya Septemba 19 na 21, 2025, na mechi za mkondo wa pili zitachezwa nyumbani kati ya Septemba 26 na 28, 2025.

Katika raundi inayofuata, mshindi wa mchezo kati ya Azam FC na Al Merriekh Bentiu atamenyana na mshindi wa mechi kati ya KMKM na AS Sport, huku mshindi wa mchezo kati ya Singida Black Stars na Rayon Sports akichuana na mshindi wa mchezo kati ya Flambeau Du Centre ya Burundi na timu kutoka Libya itakayojulikana baadaye.
Mechi za Hatua ya Awali CAFCC 2025/26 kwa Wawakilishi wa Tanzania:
-
πΈπΈ Al Merriekh Bentiu π πΉπΏ Azam FC
-
π·πΌ Rayon Sports π πΉπΏ Singida Black Stars
-
π©π― AS Sport π πΉπΏ KMKM (Zanzibar)
CHECK ALSO:
Weka maoni yako