CAF Yabadili Uwanja wa Mechi ya Marudiano ya Fainali ya CAFCC: Simba SC imejikuta katika mzozo wa kimawasiliano na mashabiki wake baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa mchezo wa hatua ya pili ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya RS Berkane utapigwa kwenye Uwanja Mpya wa Amaan Complex, Zanzibar, huku klabu hiyo ikigoma kuweka hadharani taarifa hizo kwa sasa.
Taarifa ya barua rasmi ya CAF ya Mei 14, 2025 kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Simba SC imeeleza kuwa, kutokana na tathmini ya kiufundi na hali ya mvua kwa sasa Tanzania Bara, CAF imependekeza mchezo wa mkondo wa pili uchezwe Uwanja wa Amman, Zanzibar.
CAF imesisitiza kuwa, usalama wa wachezaji, waamuzi na mashabiki pamoja na ubora wa uwanja katika msimu huu wa mvua ndio sababu kuu za kupeleka mechi visiwani humo/CAF Yabadili Uwanja wa Mechi ya Marudiano ya Fainali ya CAFCC.
CAF Yabadili Uwanja wa Mechi ya Marudiano ya Fainali ya CAFCC
Hata hivyo, katika taarifa yao ya leo Mei 15, 2025, kupitia mitandao yao ya kijamii, Simba SC wamesema:
“Taarifa rasmi kuhusu uwanja wa mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika itatolewa baada ya mchezo wa awali utakaochezwa Jumamosi Mei 17, 2025.”
Kauli hii imeibua sintofahamu kwa wanachama na mashabiki, ambao wengi wao walitegemea kuwa mechi hiyo itachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa, tikiti 12,000 za mechi hiyo tayari zimeuzwa, na uwanja wa Amaan Complex una uwezo wa kuchukua 15,000 pekee. Hali hii imezua taharuki kutokana na mashabiki wengi kuamini mechi hiyo itabaki jijini Dar es Salaam na hivyo kuongeza uwezekano wa kutokea fujo na usumbufu hasa iwapo kutakuwa na mabadiliko ya ghafla ya uwanja bila taarifa za kina.
Uwanja wa Amaan uliopo Zanzibar ni miongoni mwa viwanja vya kisasa vilivyojengwa kwa msaada wa serikali ya China. Uwanja huu umekuwa ukitumika kwa mechi kadhaa za kimataifa, lakini uwezo mdogo na tofauti za kijiografia ni changamoto zinazoweza kuathiri maandalizi ya fainali kuu/CAF Yabadili Uwanja wa Mechi ya Marudiano ya Fainali ya CAFCC.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako