CAF Yaifungia Simba Mechi Moja ya Nyumbani ya Ligi ya Mabingwa Afrika

CAF Yaifungia Simba Mechi Moja ya Nyumbani ya Ligi ya Mabingwa Afrika: SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetangaza hatua za kinidhamu dhidi ya klabu ya Simba SC ya Tanzania kufuatia tukio la utovu wa nidhamu lililotokea katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya.

Katika tukio hilo shabiki mmoja aliingia uwanjani na kuwasha moto na kukiuka kanuni za usalama za CAF. Kutokana na hali hiyo, shirikisho hilo limeamua kuifungia Simba SC kucheza mechi ya nyumbani katika mashindano ya kimataifa msimu huu bila watazamaji.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, mechi ya watani Simba SC dhidi ya Gaborone United ya Botswana, itakayochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, itachezwa bila watazamaji.

CAF Yaifungia Simba Mechi Moja ya Nyumbani ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Aidha, CAF imetoa adhabu ya mechi mbili za nyumbani kwa Simba SC, ambapo:

  • Moja itatekelezwa sasa (dhidi ya Gaborone United).

  • Ya pili imesimamishwa kwa masharti, na itatekelezwa endapo matukio ya uvunjifu wa nidhamu yatarudiwa msimu huu.

CAF Yaifungia Simba Mechi Moja ya Nyumbani ya Ligi ya Mabingwa Afrika
CAF Yaifungia Simba Mechi Moja ya Nyumbani ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Ni muhimu kusisitiza kuwa adhabu hii haihusiani na fainali dhidi ya RS Berkane, licha ya kuwepo kwa taarifa zisizo rasmi zilizodai vinginevyo.

Uamuzi huu ni onyo kwa mashabiki na uongozi wa Simba SC. Mashabiki na wadau wote wa klabu lazima waelewe kwamba utovu wa nidhamu unabeba gharama kubwa kwa timu, si tu kifedha bali hata kiushindani.

Klabu hii yenye historia ndefu barani Afrika italazimika kutafuta matokeo mazuri bila kuungwa mkono na mashabiki wake wa nyumbani jambo ambalo linaweza kuathiri ari ya wachezaji.

Simba SC sasa iko kwenye majaribio ya kinidhamu. Mashabiki na uongozi lazima wawe waangalifu ili kuepuka kurudia makosa yanayoweza kuathiri njia ya klabu kuelekea Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/2026, CAF Yaifungia Simba Mechi Moja ya Nyumbani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

CHECK ALSO:

  1. Rekodi za Simba na Yanga Ngao ya Jamii
  2. Kikosi cha Simba Leo vs Yanga 16/09/2025
  3. Kikosi cha Yanga Leo vs Simba 16/09/2025
  4. Ratiba ya Mechi za Klabu Bingwa Ulaya UEFA Leo