CAF Yaitoza TFF Faini ya Dola 10000 kwa Kuvunja Masharti ya Usalama: Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limelitoza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) faini ya dola 10,000 (sawa na takriban shilingi milioni 25 za Tanzania) kwa kushindwa kuzingatia masharti ya usalama yaliyoainishwa katika Ibara ya 82 na 83 ya Kanuni za Nidhamu za CAF, pamoja na Kanuni za 24 na 28 za Kanuni za Usalama.
Adhabu hiyo ilitolewa na Bodi ya Nidhamu ya CAF kufuatia uvunjifu wa usalama wakati wa mechi ya Tanzania dhidi ya Burkina Faso kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024. Mchezo huo uliomalizika kwa Tanzania kupata ushindi wa mabao 2-0, uligubikwa na utovu wa nidhamu wa baadhi ya mashabiki.
CAF Yaitoza TFF Faini ya Dola 10000 kwa Kuvunja Masharti ya Usalama
Mbali na TFF, CAF pia imelipiga faini Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kwa matukio yaliyotokea wakati wa michuano hiyo:
-
Dola 5,000 (takriban Tsh. Milioni 12) kwa msongamano wa watu (stampede) na kuingia bila idhini.
-
Dola 10,000 (takriban Tsh. Milioni 25) kwa kosa la kuwashambulia wafanyakazi wa CAF na wageni.

Umuhimu wa Kuzingatia Sheria
CAF imesisitiza kuwa suala la usalama wa wachezaji, waamuzi na mashabiki ni jambo la msingi, na kushindwa kuzingatia sheria hizo kunaweza kuathiri heshima ya mashindano. Vyama wanachama wa kandanda vinahimizwa kuhakikisha vinafuatwa ipasavyo taratibu za kiusalama ili kuepuka aina hii ya vikwazo.
Tukio hili liwe onyo kwa wadau wote wa soka nchini. Mashabiki wametakiwa kudumisha nidhamu viwanjani, huku TFF ikiboresha utekelezaji wa taratibu za usalama ili kulinda taswira ya soka la Tanzania katika mashindano ya kimataifa/CAF Yaitoza TFF Faini ya Dola 10000 kwa Kuvunja Masharti ya Usalama.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako