CAF Yatangaza Orodha Rasmi ya Waamuzi wa AFCON 2025

CAF Yatangaza Orodha Rasmi ya Waamuzi wa AFCON 2025, SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetangaza rasmi orodha ya waamuzi na viongozi watakaochezesha michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, itakayofanyika nchini Morocco kuanzia Desemba mwaka huu.

CAF Yatangaza Orodha Rasmi ya Waamuzi wa AFCON 2025

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CAF, waamuzi wote walioteuliwa wanapaswa kuripoti mjini Cairo, Misri, ifikapo Novemba 21 kwa ajili ya kambi maalum ya maandalizi ya maandalizi kabla ya kuanza kwa michuano hiyo muhimu ya Afrika.

Miongoni mwa waamuzi walioteuliwa, Burundi ina mwakilishi mmoja, mwamuzi Pacifique Ndabihawenimana, ambaye ameonyesha kiwango cha juu cha kuchezesha mechi za kimataifa.

Hii itakuwa AFCON ya nne kwa Ndabihawenimana, baada ya kushiriki kama mwamuzi katika mashindano ya 2019, 2021, na 2023. Uteuzi wake unaonyesha ukuaji wa Burundi katika sekta ya wasimamizi wa soka barani Afrika.

Kwa upande wa Tanzania, hakuna waamuzi wala viongozi walioteuliwa katika mchujo wa mwaka huu, jambo lililozua maswali kuhusu maendeleo ya waamuzi wa ndani na msimamo wa nchi katika nyanja ya soka la Afrika.

CAF Yatangaza Orodha Rasmi ya Waamuzi wa AFCON 2025
CAF Yatangaza Orodha Rasmi ya Waamuzi wa AFCON 2025

Wataalamu wa soka wamependekeza Tanzania iongeze uwekezaji katika mafunzo, maadili na ubora wa waamuzi wake ili kujihakikishia uwakilishi wao katika michuano mikubwa kama vile Kombe la Mataifa ya Afrika na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kambi hiyo ya maandalizi itakayofanyika mjini Cairo, inalenga kutoa mafunzo ya kina kuhusu matumizi ya teknolojia ya VAR, marekebisho ya sheria za mchezo, na kuboresha maandalizi ya kisaikolojia na kimwili ya waamuzi wote watakaoshiriki Kombe la Mataifa ya Afrika 2025.

CAF imesisitiza umuhimu wa uadilifu, uwazi na viwango vya juu vya waamuzi ili kuhakikisha mashindano hayo yanaendeshwa kwa haki na heshima/CAF Yatangaza Orodha Rasmi ya Waamuzi wa AFCON 2025.

CHECK ALSO:

  1. Timu Zilizofuzu Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/26 CAF
  2. Ratiba ya CAF Klabu Bingwa Afrika 2025/2026
  3. Patrick Mabedi Kocha Mkuu wa Muda Yanga SC
  4. Pyramids FC Mabingwa wa CAF Super Cup 2025