CAF Yatangaza Tarehe Rasmi ya Droo ya Makundi Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika 2025/26

CAF Yatangaza Tarehe Rasmi ya Droo ya Makundi Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika 2025/26: SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetangaza rasmi kuwa droo ya hatua ya makundi kwa ajili ya mashindano ya vilabu kuu barani Afrika (CAF Champions League na CAF Confederation Cup) itafanyika Jumatatu, Novemba 3, 2025, Johannesburg, Afrika Kusini.

CAF Yatangaza Tarehe Rasmi ya Droo ya Makundi Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika 2025/26

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CAF:

  • Droo ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) itaanza saa 11:00 GMT, sawa na saa 2:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki (EAT).

  • Droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) itafuata saa 12:00 GMT, ambayo ni saa 3:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki.

Sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari rasmi vya CAF na mitandao ya kijamii, ili kuruhusu mashabiki kote barani Afrika kufuatilia matokeo ya droo/CAF Yatangaza Tarehe Rasmi ya Droo ya Makundi Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika 2025/26.

Klabu nne za Tanzania—Simba SC, Yanga SC, Azam FC, na Singida Black Stars—zinatarajiwa kufuatilia kwa karibu droo hiyo muhimu.

CAF Yatangaza Tarehe Rasmi ya Droo ya Makundi Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika 2025/26
CAF Yatangaza Tarehe Rasmi ya Droo ya Makundi Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika 2025/26

Timu hizi zinachuana vikali katika awamu ya awali ya shindano hilo, zikitarajia kutinga hatua ya makundi kwa msimu wa 2025/26.

  • Simba SC na Yanga SC zinashiriki katika Ligi ya Mabingwa Afrika,
  • Wakati Azam FC na Singida Black Stars zikiwa zinashiriki kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Matokeo ya droo hiyo yatakuwa na umuhimu mkubwa kwa maandalizi ya vilabu hivi, hasa katika kupanga mikakati ya kiufundi na safari za kimataifa.

Droo ya hatua ya makundi inaashiria mwanzo wa hatua muhimu zaidi ya mashindano hayo, ambapo klabu bora zaidi barani Afrika zinachuana. Timu hizo zimegawanywa katika makundi manne, kila moja ikiwa na vilabu vinne.

Timu mbili za juu katika kila kundi huingia hatua ya mtoano (robo fainali). Kwa vilabu vya Afrika Mashariki hasa Tanzania hatua hii ni fursa ya kudhihirisha ukuaji wa soka la ukanda na ubora wa ligi ya taifa.

CHECK ALSO:

  1. Kikosi cha Azam FC vs KMKM Leo 24/10/2025
  2. Matokeo Azam FC vs KMKM Leo 24/10/2025
  3. CAF Ranking 2025/2026 Best Football Clubs in Africa
  4. Orodha ya Vilabu Bora Afrika CAF 2025 Club Ranking