CAS Yakiri Kupokea Barua Rasmi ya Yanga dhidi ya Bodi ya Ligi: TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC wanakabiliwa na mashtaka Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imekiri kupokea barua rasmi kutoka kwa Klabu ya Yanga Afrika kuhusu kesi yake ya madai dhidi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Klabu ya Simba SC.
Taarifa ya CAS imewapa siku 10 washtakiwa (TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC) kujiandaa na utetezi wao kabla ya kuanza kusikilizwa rasmi. Kesi hiyo, nambari ya kumbukumbu CAS 2025/A/11298, inatarajiwa kushughulikiwa haraka ili kuhakikisha uamuzi wa haki.
Hadi sasa hoja kuu za Yanga Afrika katika kesi hiyo hazijaeleweka kikamilifu, lakini ni wazi klabu hiyo imeamua kufuata hatua za kimataifa kuhakikisha haki inatendeka. Uamuzi huu unaweza kuleta athari kubwa kwa mustakabali wa soka la Tanzania hasa kwa vilabu na wadau wa soka nchini walioathirika.
CAS Yakiri Kupokea Barua Rasmi ya Yanga dhidi ya Bodi ya Ligi

Mashabiki na wachambuzi wa soka wanasubiri kwa hamu jinsi kesi hii itakavyotokea na ni uamuzi gani CAS, chombo kinachotambulika kimataifa cha kusuluhisha mizozo ya michezo itatoa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako