CECAFA Kagame Cup 2025 Timu 12 Zathibitisha, Kuanza Septemba 2 hadi 15

CECAFA Kagame Cup 2025 Timu 12 Zathibitisha, Kuanza Septemba 2 hadi 15: Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limethibitisha orodha ya timu 12 zitakazoshiriki michuano ya CECAFA Kagame Cup 2025, itakayoanza Septemba 2 hadi 15 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mashindano wa CECAFA, Yusuf Mossi, maandalizi yapo katika hatua za mwisho, na timu zote zinatarajiwa kuwasili Dar es Salaam ifikapo Agosti 30, 2025. Droo ya hatua ya makundi itafanyika Agosti 26, 2025.

CECAFA Kagame Cup 2025 Timu 12 Zathibitisha, Kuanza Septemba 2 hadi 15

Timu Shiriki CECAFA Kagame Cup 2025

  1. Singida Black Stars FC (Tanzania)
  2. Mogadishu City Club (Somalia)
  3. APR FC (Rwanda)
  4. Vipers SC (Uganda)
  5. El Merriekh SC Bentiu (Sudan Kusini)
  6. Mlandege SC (Zanzibar)
  7. Kenya Police FC (Kenya)
  8. Flambeau du Centre (Burundi)
  9. Garde Cotes FC (Djibouti)
  10. Ethiopian Coffee SC (Ethiopia)
  11. Al Hilal Omdurman (Sudan)
  12. Al Ahly SC Wad Madani (Sudan)
CECAFA Kagame Cup 2025 Timu 12 Zathibitisha, Kuanza Septemba 2 hadi 15
CECAFA Kagame Cup 2025 Timu 12 Zathibitisha, Kuanza Septemba 2 hadi 15

Katika michuano ya mwaka jana, Red Arrows FC ya Zambia ilitawazwa kuwa mabingwa baada ya kuifunga APR FC ya Rwanda katika fainali iliyofanyika kwenye Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo ya watani, Tanzania itaongozwa na Singida Black Stars FC, ambao wanatarajiwa kutumia fursa ya nyumbani kuonesha vipaji vyao. Mashabiki pia wanatarajia ushindani mkali kutoka kwa timu zenye nguvu za kikanda kama vile Vipers SC ya Uganda na APR FC ya Rwanda.

Kwa ujumla michuano ya CECAFA Kagame Cup 2025 inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na kuzikutanisha klabu bora kutoka Afrika Mashariki na Kati huku Tanzania ikiwa kitovu cha burudani ya soka kwa wiki mbili mfululizo.

SOMA PIA:

  1. MATOKEO ya Taifa Stars Leo Vs Morocco 22/08/2025
  2. Kikosi cha Taifa Stars Leo Vs Morocco 22/08/2025
  3. CV ya Frank Assinki Mchezaji wa Yanga SC 2025/2026
  4. Frank Assinki Ajiunga na Yanga SC Kutoka Singida Black Stars