Chama Ajiunga na Singida Black Stars kwa Mkataba wa Mwaka Mmoja | Klabu ya Singida Black Stars imepiga hatua kubwa kwenye soko la usajili baada ya kutangaza kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka Zambia, Clatous Chama ambaye amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Chama Ajiunga na Singida Black Stars kwa Mkataba wa Mwaka Mmoja
Chama anayesifika kwa uwezo wake wa kutengeneza nafasi na kufunga mabao muhimu, anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika soka la Afrika. Nyota huyo wa Zambia ametamba katika vilabu kadhaa na sasa ana jukumu la kuimarisha kikosi cha kocha Miguel Gamondi.
Gamondi anaripotiwa kumuona Chama kama nguzo muhimu ya mafanikio ya Singida Black Stars katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) pamoja na Kombe la Shirikisho la CAF.

Ujio wa Chama unatarajiwa kuiongezea nguvu safu ya ushambuliaji ya Singida Black Stars, na mashabiki wanatamani kuona namna atakavyoshirikiana na wachezaji wengine wa kikosi hicho kipya chenye lengo la kuwiana vikali msimu huu.
Kwa mashabiki na wachambuzi wa soka usajili huu unaonekana kuwa ni ishara ya dhamira ya klabu ya Singida Black Stars ya kujenga timu yenye ushindani mkubwa katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
SOMA PIA:
Weka maoni yako