CRDB Bank Yakanusha Madai ya Kutolipa Zawadi ya Ubingwa wa Federation Cup 2023/2024

CRDB Bank Yakanusha Madai ya Kutolipa Zawadi ya Ubingwa wa Federation Cup 2023/2024, Benki ya CRDB Yatoa Taarifa Rasmi Kuhusu Malipo ya Kombe la Shirikisho 2023/2024 | Inathibitisha malipo kwa TFF kwa mujibu wa Mkataba

Benki ya CRDB imetoa taarifa rasmi na kufafanua kuwa imetekeleza kikamilifu wajibu wake wa kifedha kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu udhamini wa Kombe la Shirikisho la CRDB kwa msimu wa 2023/2024.

CRDB Bank Yakanusha Madai ya Kutolipa Zawadi ya Ubingwa wa Federation Cup 2023/2024

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, benki imesema:

“Benki ilikwisha tekeleza kikamilifu wajibu wake wa kifedha kwa TFF kama sehemu ya makubaliano ya udhamini wa mashindano haya, malipo yote ya msimu uliopita yalifanyika kwa TFF kwa mujibu wa mkataba baina ya Benki ya CRDB na TFF.”

CRDB Bank Yakanusha Madai ya Kutolipa Zawadi ya Ubingwa wa Federation Cup 2023/2024
CRDB Bank Yakanusha Madai ya Kutolipa Zawadi ya Ubingwa wa Federation Cup 2023/2024

Kauli hiyo ya CRDB inafuatia taarifa ya Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe, ambaye alidai kuwa klabu yake haijapokea fedha yoyote ya zawadi wala zawadi ya michuano ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita.

Kauli hii ilizua mjadala mkali miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka, wakitaka kujua fedha hizo zimekwenda wapi ikiwa tayari mfadhili ametimiza wajibu wake.

CHECK ALSO:

  1. Sakata la Dabi ya Kariakoo Juni 15, Tiketi za Machi 8 Zitatumika
  2. Jezi Mpya ya FC Bayern Munich Kwa Msimu wa 2025/2026
  3. Taifa Stars Kukipiga na Eswatini Katika Mchezo wa COSAFA Kundi C
  4. Usajili wa Clement Mzize Kuelekea Zamalek Wasitishwa