Diogo Jota Afariki Dunia kwa Ajali ya Barabarani Akiwa na Umri wa Miaka 28 | Jota afariki akiwa na umri wa miaka 28 baada ya ajali ya gari nchini Uhispania
Ulimwengu wa soka upo katika majonzi kufuatia kifo cha mshambuliaji Diogo Jota ambaye inasemekana alifariki katika ajali mbaya ya gari akiwa na umri wa miaka 28. Tukio hilo limetokea nchini Hispania na limewashangaza mashabiki, wanamichezo na jamii kwa ujumla.
Diogo Jota Afariki Dunia kwa Ajali ya Barabarani Akiwa na Umri wa Miaka 28
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Jota aliaga dunia siku chache tu baada ya kufunga ndoa na kuacha mjane na watoto watatu. Vifo vya ghafla namna hii huwa vya kusikitisha hasa vinapotokea pale ambapo maisha mapya kwa mchezaji yalikuwa yanaanza.

Diogo Jota alikuwa mchezaji anayeheshimika sana ndani na nje ya uwanja. Aliwavutia wengi kwa uwezo wake wa soka, uadilifu wake, na kujitolea kwake kwa timu na mashabiki wake. Kwa mashabiki wa soka, Jota hakuwa mchezaji wa kuvutia tu, bali pia mfano wa kuigwa.
Familia yake, marafiki wa karibu, na mashabiki wa soka duniani kote wanaomboleza kuondokewa na mpendwa wao. Ni hasara kubwa ambayo haiwezi kufutika katika historia ya soka.
CHECK ALSO:








Weka maoni yako