Droo ya CAF 2025/26 Kufanyika Azam TV, Agosti 9 Saa 8 Mchana: Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza rasmi kuwa droo ya hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika 2025/2026 itafanyika Agosti 9, 2025, saa 8:00 mchana. Saa za Dar es Salaam.
Droo ya CAF 2025/26 Kufanyika Azam TV, Agosti 9 Saa 8 Mchana
Tukio hili muhimu litafanyika katika studio za Azam TV jijini Dar es Salaam, Tanzania. Hii ni hatua kubwa kwa Tanzania katika kuandaa moja ya matukio muhimu katika kalenda ya soka barani Afrika, kuonyesha heshima ya nchi hiyo katika tasnia ya utangazaji na usimamizi wa michezo.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, vyama vyote vya soka wanachama wa CAF vimewasilisha majina ya klabu zao zitakazoshiriki michuano hiyo mikubwa. Hata hivyo, Libya ndiyo nchi pekee ambayo haijakamilisha mchakato huo, ikiwa imeomba muda wa nyongeza kutokana na ugumu wa mechi za kufuzu kwa timu zake, zilizofanyika nchini Italia.

CAF ilithibitisha kuwa mikataba yote ya kiufundi na kisheria kuhusiana na maandalizi ya droo hiyo imesainiwa na kwamba taratibu zote zimekamilika kwa mafanikio.
Vilabu shiriki vimeshauriwa kufuatilia kwa ukaribu droo hii kupitia matangazo ya moja kwa moja ya Azam TV, huku mashabiki wakihimizwa kufuatilia droo hiyo, kwani itawapa taswira ya mapema ya safari ya klabu zao barani Afrika msimu ujao.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako