Droo ya CAF 2025/26 Kufanyika Tanzania Mwezi Agosti

Droo ya CAF 2025/26 Kufanyika Tanzania Mwezi Agosti: CAF yathibitisha. Droo za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho zitafanyika nchini Tanzania mwezi Agosti 2025/26.

Droo ya CAF 2025/26 Kufanyika Tanzania Mwezi Agosti

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza rasmi kuwa droo za michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2025/2026 zitafanyika katikati ya Agosti 2025 nchini Tanzania.

Uamuzi huu ni heshima kubwa kwa Tanzania na ni kielelezo cha hali ya nchi hiyo kukua katika medani ya soka kimataifa. Tukio hili linalosubiriwa kwa hamu kubwa linatarajiwa kuvutia wachezaji wengi wa soka kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Majina ya klabu yawasilishwe ndani ya siku nne

Droo ya CAF 2025/26 Kufanyika Tanzania Mwezi Agosti
Droo ya CAF 2025/26 Kufanyika Tanzania Mwezi Agosti

CAF imevikumbusha vyama vyote wanachama kuwa zimesalia siku nne pekee hadi tarehe rasmi ya kuwasilisha majina ya vilabu kwa ajili ya kushiriki mashindano ya CAF kwa msimu wa 2025/26. Hii ni hatua muhimu kabla ya kuanza rasmi kwa ratiba ya mechi.

CAF imetoa muda maalum kwa Libya kuwasilisha jina la klabu itakayoshiriki mashindano hayo, kutokana na ukweli kwamba fainali ya kumpata bingwa wa taifa itafanyika nchini Italia.

CHECK ALSO:

  1. Jean Ahoua Arejea Simba SC Kujiandaa na Msimu Mpya
  2. Utajiri Wa Cristiano Ronaldo Wafika Bilioni Dola za Marekani
  3. CV ya Neo Maema Mchezaji Mpya wa Simba SC 2025/2026
  4. Jonathan Sowah Ajiunga na Simba SC Kutoka Singida Black Stars