Droo ya Ligi ya Mabingwa na Shirikisho CAF 2025/2026

Droo ya Ligi ya Mabingwa na Shirikisho CAF 2025/2026: CAF Yatangaza Dar es Salaam kuwa Mwenyeji wa Droo ya Klabu Bingwa Afrika 2025/2026.

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limethibitisha rasmi kuwa droo ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2025/2026 itafanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, droo hiyo itafanyika kabla ya Agosti 12, 2025, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya awali ya mashindano makubwa ya vilabu barani Afrika.

Droo ya Ligi ya Mabingwa na Shirikisho CAF 2025/2026

Awamu ya kwanza ya mechi za mashindano hayo itakuwa Septemba 19-21, 2025 huku mechi za marudiano ikiwa ni Septemba 26-28, 2025.

Ratiba ya Awamu ya Kwanza ya Mashindano:

  • 🗓️ Mechi za Kwanza: Septemba 19–21, 2025

  • 🔁 Mechi za Marudiano: Septemba 26–28, 2025

Droo ya Ligi ya Mabingwa na Shirikisho CAF 2025/2026
Droo ya Ligi ya Mabingwa na Shirikisho CAF 2025/2026

Uamuzi wa CAF kufanya droo hiyo nchini Tanzania ni ishara ya kuimarika kwa nafasi ya Tanzania kwenye ramani ya soka Afrika, huku vilabu kama Simba SC na Young Africans SC (Yanga) vikiendelea kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Droo ya CAF msimu wa 2025/2026 ni tukio la kihistoria kwa Tanzania. Tukio hili litasaidia kuimarisha sifa ya nchi katika soka la Afrika na kuzipa klabu za ndani fursa ya kujiandaa mapema kwa mashindano ya kimataifa. Mashabiki na wahusika wanashauriwa kufuatilia kwa karibu tangazo rasmi la CAF kuhusu tarehe kamili ya droo.

CHECK ALSO:

  1. Zawadi ya Mashindano ya CAF CHAN 2024/2025
  2. Wachezaji wa Kigeni Ndani ya Simba SC 2025/2026
  3. Mbeya City FC Yafanya Maboresho ya Kikosi, Yawaaga Wachezaji 9 na Kusajili 3
  4. JKT Tanzania Yaachana na Wachezaji 7, Dirisha Kubwa La Usajili 2025/26