Edd el Hajj 2025 Tanzania, BAKWATA Yatangaza Rasmi Tarehe 7 Juni

Edd el Hajj 2025 Tanzania, BAKWATA Yatangaza Rasmi Tarehe 7 Juni: BAKWATA Yatangaza Rasmi Tarehe ya Eid Al-Adh’ha 2025 | Maombi ya Kitaifa Kufanyika Jijini Dar es Salaam

Dar es Salaam – Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kuwa sikukuu ya Eid Al-Adh’ha 2025 itaadhimishwa Jumamosi Juni 7, 2025. Tangazo hilo limetolewa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dk Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana, kupitia ofisi ya BAKWATA.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, sherehe za Eid al-Adh’ha mwaka huu kitaifa zitafanyika katika mkoa wa Dar es Salaam, ambapo Swala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohammed VI, uliopo makao makuu ya BAKWATA Kinondoni, kuanzia saa 1:30 asubuhi.

Baada ya swala ya Iddi kutafanyika Baraza rasmi la Eid litakalohudhuriwa na viongozi wa dini, viongozi wa serikali na waumini mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Edd el Hajj 2025 Tanzania, BAKWATA Yatangaza Rasmi Tarehe 7 Juni

Edd el Hajj 2025 Tanzania, BAKWATA Yatangaza Rasmi Tarehe 7 Juni
Edd el Hajj 2025 Tanzania, BAKWATA Yatangaza Rasmi Tarehe 7 Juni

Eid al-Adha, maarufu kama “Sikukuu ya Sadaka,” ni moja ya sherehe mbili muhimu zaidi katika Uislamu. Inaadhimishwa kumkumbuka Nabii Ibrahim (as) kwa utiifu wake kwa Mwenyezi Mungu katika tukio ambalo alikuwa tayari kumchinja mwanawe. Siku hii inaambatana na ibada ya kutoa dhabihu za wanyama kwa ajili ya sadaka, hasa kwa Waislamu ambao wana uwezo wa kuhiji Makka.

Bakwata inawahimiza waumini wote wa Kiislamu kufuata taratibu rasmi za ibada, kutoa sadaka kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, na kusherehekea kwa amani. Pia anaikumbusha jamii ya Kiislamu kujenga moyo wa ukarimu kwa wale wanaohitaji ikiwa ni ishara ya mshikamano na upendo.

CHECK ALSO: