FA Yaomba Adhabu Kali kwa Kipa wa Millwall Liam Roberts

FA Yaomba Adhabu Kali kwa Kipa wa Millwall Liam Roberts Baada ya majeraa mabaya ya Mateta.

FA Yaomba Adhabu Kali kwa Kipa wa Millwall Liam Roberts

Chama cha Soka (FA) kimewasilisha ombi la kurefusha marufuku ya mechi tatu aliyowekewa kipa wa Millwall Liam Roberts baada ya kumjeruhi vibaya mshambuliaji wa Crystal Palace Jean-Philippe Mateta.

Katika mechi ya raundi ya tano ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Selhurst Park Jumamosi, Roberts alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya nane kufuatia tukio hilo hatari. Mateta alipata jeraha baya kwenye sikio lake la kushoto lililohitaji kushonwa nyuzi 25.

FA Yaomba Adhabu Kali kwa Kipa wa Millwall Liam Roberts
FA Yaomba Adhabu Kali kwa Kipa wa Millwall Liam Roberts

FA inasema marufuku ya mechi tatu ni ndogo

FA imesema kufungiwa mechi tatu ni adhabu ndogo na imetuma malalamiko rasmi kwa Chama cha Soka ili kutathmini uwezekano wa kurefusha adhabu ya golikipa huyo.

Millwall wamethibitisha kupinga madai hayo na kuendelea kumuunga mkono Liam Roberts, huku wakilaani vikali unyanyasaji wa mtandaoni alioupata kipa wao kufuatia tukio hilo.

Bado haijabainika ni adhabu gani zaidi inaweza kutolewa iwapo FA itashinda kesi yake. Mashabiki wa kandanda wanasubiri uamuzi wa mwisho kutoka kwa bodi inayosimamia, ambayo itaamua ikiwa marufuku ya Roberts itaongezwa au kubaki kama ilivyo.

CHECK ALSO: