Gharama za Kujisajili Mitihani ya NECTA

Gharama za Kujisajili Mitihani ya NECTA

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) husimamia mitihani mbalimbali nchini, kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi elimu ya juu. Kwa wale wanaojiandaa kufanya mtihani wowote ule unaosimamiwa na NECTA, ni muhimu kuwa na uelewa wa kina kuhusu gharama za usajili ili kuhakikisha mchakato unaenda vizuri na kuepuka usumbufu wowote unaoweza kujitokeza.

Hapa tumekuletea muongozo kamili na wa kuhusu ada za usajili wa mitihani mbalimbali inayotolewa na NECTA. Taarifa hizi zitakusaidia kuelewa vyema gharama zinazohusika na kufanya maandalizi stahiki kabla ya kuanza mchakato wa usajili. Ni muhimu kutambua kuwa ada hizi zinaweza kubadilika, hivyo inashauriwa kutembelea tovuti rasmi ya NECTA (www.necta.go.tz) ili kupata taarifa zilizosasishwa.

Aina za Mitihani na Ada za Usajili wa Mitihani ya NECTA

Baraza lamitihani Tanzania NECTA husimamia mitihani mbalimbali kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi elimu ya juu. Ada za usajili hutofautiana kulingana na aina ya mtihani. Hapa chini kuna orodha ya mitihani na ada zake:

Aina ya MtihaniAda ya Usajili wa KawaidaAda ya Usajili wa Kuchelewa
Cheti cha Elimu ya Msingi (kwa Kiingereza)TZS 15,000N/A
Mtihani wa Maarifa (QT)TZS 30,000TZS 40,000
Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE)TZS 50,000TZS 65,000
Cheti cha Juu cha Elimu ya Sekondari (ACSEE)TZS 50,000TZS 65,000
Cheti cha Mwalimu Daraja ATZS 50,000TZS 65,000
Stashahada ya Elimu ya SekondariTZS 50,000TZS 65,000

Gharama za Kujisajili Mitihani ya NECTA

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Tarehe za Kujiandikisha Mitihani ya Taifa ya NECTA
  2. Ajira Portal: Jinsi ya Kujisajili na Kuomba Nafasi za Kazi Serikalini 2024
  3. Orodha ya Shule za Sekondari Mkoa wa Pwani
  4. Michepuo Ya Sanaa Kidato Cha Tano
  5. Sababu za Ada Kubwa Katika Shule Binafsi Tanzania
  6. Muonekano wa Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne