Haya hapa matokeo ya kidato cha nne 2025

Haya hapa matokeo ya kidato cha nne 2025: NECTA Yatangaza Matokeo ya Kidato cha Nne 2025, Ufaulu Waongezeka.

Haya hapa matokeo ya kidato cha nne 2025

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne (CSEE) wa mwaka 2025. Mtihani huo ulifanyika kuanzia Novemba 17, 2025, na matokeo yametangazwa leo Jumamosi, Januari 31, 2026.

Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohammed, alisema kuwa matokeo yanaonesha ongezeko la ufaulu ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Kwa mujibu wa NECTA, jumla ya watahiniwa 569,883 walishiriki mtihani huo wakiwa wamesajiliwa katika shule 5,864 kote nchini. Aidha, watahiniwa wa kujitegemea 25,927 waliosajiliwa katika vituo 813 pia walifanya mtihani huo.

Haya hapa matokeo ya kidato cha nne 2025
Haya hapa matokeo ya kidato cha nne 2025

Taarifa ya NECTA ya Novemba 16, 2025, ilibainisha kuwa idadi ya watahiniwa wa mwaka 2025 imeongezeka kwa asilimia 7.67 ikilinganishwa na mwaka 2024. Kati ya watahiniwa wa shule 569,914 waliosajiliwa, wavulana walikuwa 266,024 sawa na asilimia 47, huku wasichana wakiwa 303,859 sawa na asilimia 53.

HAYA HAPA MATOKEO

Mahudhurio katika mtihani yalikuwa ya juu, yakifikia asilimia 97.5, sawa na watahiniwa 555,606 waliofanya mtihani.

Takwimu za NECTA zinaonesha kuwa ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 2.61 na kufikia asilimia 94.98. Jumla ya watahiniwa 526,620 wamefaulu kwa kupata daraja la I, II, III na IV. Vilevile, idadi ya watahiniwa waliopata daraja la kwanza hadi la tatu imeongezeka, ambapo wanafunzi 255,404 sawa na asilimia 46.1 wamefikia viwango hivyo.

CHECK ALSO:

  1. Baraza la mitihani NECTA Kutangaza Matokeo ya Kidato cha Nne Leo
  2. Matokeo ya Kidato cha Nne Kutangaza Januari 31, 2026
  3. NECTA Kutangaza Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 Januari 31, 2026
  4. Matokeo ya Kidato cha Nne 2025/2026 CSEE NECTA