HESLB Yafungua Dirisha la Mikopo 2025/26, Sh916.7 Bilioni Kununufaisha Wanafunzi 252773

HESLB Yafungua Dirisha la Mikopo 2025/26, Sh916.7 Bilioni Kununufaisha Wanafunzi 252773 | HESLB Yatangaza Muda wa Kuomba Mikopo kwa Mwaka wa Masomo 2025/26: Zaidi ya Wanafunzi 252,000 Watanufaika.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefungua rasmi muda wa maombi kwa wanafunzi wa elimu ya sekondari na vyuo kwa mwaka wa masomo 2025/26. Maombi yamepangwa kuanza Juni 15 hadi Agosti 31, 2025.

HESLB Yafungua Dirisha la Mikopo 2025/26, Sh916.7 Bilioni Kununufaisha Wanafunzi 252773

Kwa mwaka huu wa masomo, jumla ya shilingi bilioni 916.7 zimetengwa kugharamia mikopo ya wanafunzi 252,773 kati yao 88,320 ni wa mwaka wa kwanza. Hii ni pamoja na diploma, bachelor’s, diploma ya juu katika mafunzo ya vitendo ya kisheria, uzamili, na wanafunzi wa ufadhili wa Samia.

Katika uzinduzi wa mwongozo wa utoaji wa mikopo na ufadhili wa masomo uliofanyika Juni 6, 2025, mjini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo, amewataka wanafunzi, wazazi, na walezi kusoma miongozo hiyo kwa makini kabla ya kujaza fomu za maombi. Alisisitiza umuhimu wa taarifa zilizomo ili waombaji waelewe vigezo, masharti na hatua zote zinazohusika katika uombaji mikopo.

HESLB Yafungua Dirisha la Mikopo 2025/26, Sh916.7 Bilioni Kununufaisha Wanafunzi 252773
HESLB Yafungua Dirisha la Mikopo 2025/26, Sh916.7 Bilioni Kununufaisha Wanafunzi 252773

Aidha, Prof.Nombo aliwaonya wanafunzi wanaotumia huduma za mtandao kwenye vituo vya huduma (cybercafés) kuhakikisha wanapata taarifa zao za mikopo badala ya kuwaacha watumishi wa kituo hicho kufuatilia taarifa hizo nyeti.

Katika kipindi cha miaka minne (2020/21 hadi 2024/25), serikali imeendelea kuongeza bajeti ya mikopo, kutoka shilingi bilioni 464 mwaka 2021 hadi shilingi bilioni 787 mwaka 2024/25. Kwa mwaka ujao wa masomo unaoanza Oktoba 2025, bajeti imeongezeka na kufikia shilingi bilioni 916.7, ikiwa ni ongezeko kubwa linalolenga kupanua fursa za elimu ya juu kwa Watanzania.

Aidha, wanafunzi 164,453 wanaoendelea na masomo nao wataendelea kunufaika na mikopo. Vilevile, mpango wa Samia Scholarship uliozinduliwa mwaka wa masomo 2022/23 kwa wanafunzi waliopata daraja la juu katika masomo ya sayansi, hadi sasa umewanufaisha wanafunzi 3,186 wa shahada ya kwanza na 80 wa uzamili, ukiwa na thamani ya shilingi bilioni 16.8.

Aidha, wanafunzi 18,000 wa stashahada wanatarajiwa kupatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 64, hatua inayolenga kukuza ujuzi wa ufundi kwa vijana wa Kitanzania.

CHECK ALSO:

  1. Haya Hapa Matokeo Kidato cha Sita 2025 NECTA
  2. TAMISEMI Second Selection Form Five 2025 to 2026
  3. Sifa za Kujiunga na Chuo cha Bandari 2025/2026
  4. Tarehe ya Mwisho ya Maombi ya Mkopo HESLB, Loan Application Deadline 2025/2026